Zari: Nimeachana na Diamond

Diamond na Zari
Maelezo ya picha,

Diamond na Zari

Unaonekana uhusiano wa wapenzi maarufu Afrika Mashariki yaani msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz na mfanya biashara wa Uganda Zari Hassan umefika ukingoni.

Zari Hassan ametangaza kuachana na mzazi mwenzake, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz baada ya kuwapo kwa tuhuma nyingi kuhusu mwanamuziki huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine.

Mashabiki wa Zari wamepokea habari hizo kwa mshangao na hisia tofauti wakituma ujumbe kwenye ukurasa wake.

Maelezo ya picha,

.

Maelezo ya picha,

.

Maelezo ya picha,

.

Diamond ni baba wa watoto wawili wa Zari ambaye ameoenakana kunyamaza kwa muda baada ya mpenziwe Diamond kukiri hadharani kudanganya katika uhusiano wao na kupata mtoto na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto.

Tangu hilo litokee mambo hayajakuwa shwari kati ya hao wawili.

Zari ametangaza uamuzi wa kuachana na Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema baada ya tuhuma nyingi dhidi ya mpenzi wake kuwa na wanawake wengine kila mara ameamua kuulinda utu wake na kuachana naye.

Japo ameendelea na kusema "tunatengana kama wapenzi na sio kama wazazi".

Diamond bado hajaweka wazi upande wake na kumjibu Zari. Bali katika ukurasa wake wa Instagram aliweka video ikionyesha akipokea tuzo yake kutoka Sound City.

Wakati Diamond alipokiri kuwa na uhusiano mwingine nje na mwanamitindo Hamisa na kupata mtoto naye , ilikuwa mwanzo wa vita vya mitandaoni na kuzua uvumi kwamba huenda wataachana.

Habari za penzi lao kuisha zilizusha madai kwamba hatua hiyo itaathiri mikataba ya mamilioni ya fedha waliotia saini ikiwemo kampuni kadhaa.