Yaya afariki baada ya kuachwa kulala nje na mbwa Malaysia

Adelina sat outside her employer's home in Malaysia Haki miliki ya picha Steven Sim Office
Image caption Adelina akiwa nje ya nyumba ya mwajiri wake Malaysia

Yaya mmoja nchini Malaysia ambaye alidhulumiwa na mwajiri wake kwa kumlazimisha kulala nje na mbwa amefariki dunia

Yaya huyo kwa jina Adelina alitokea nchini Indonesia na kwenda kuifanyia kazi familia moja huko Panang, Malaysia.

Waajiri wake wanalaumiwa kwa kutompa chakula na kutojali kuwa vidonda vyake vingepata matibabu.

Adelina aliokolewa tarehe 10 Februari baada ya jirani kuripoti hali yake kwa mwanasiasa Steven Sim.

Alilazwa hospitalini siku ya Jumapili ambayo alifariki dunia baadaye.

Mwanamke wa umri wa miaka 36 na nduguye kwa sasa wanachunguzwa kwa kushukiwa kuua kwa mujibu wa polisi wa Malaysia.

Mama yao wa miaka 60 pia amekamatwa na kwa sasa yuko kwenye kizuizi cha polisi.

Haki miliki ya picha Migrant Care
Image caption Adelina alikuwa na vidonda kwenye mikono na miguu

Kifo cha Adelina na jinsi alivyotendewa ni jambo limesababisha ghadhabu kubwa nchini Malaysia

Inaripotiwa kuwa Adelina alikuwa na vidonda na hakuwa ametibiwa hali ilichangia kufeli kwa viungo vya mwili.

Waziri wa mashauri ya chi kigeni wa Indonesia Ratno Marsudi alisema alitaka Adelina apate haki.

Malaysia ni moja ya nchi zinazowachukuaa wafanyakazi wengi zaidi Asia ambapo wafanyazi uhamia huko kufanya kazi na malipo ya chini.

Kuna takriba raia milioni 2.5 wa Indonesia wanaofanya kazi nchini Malaysia na nusu yao wanafanya kazi kinyume cha sheria.

Wafanyakazi wengine hutokea nchini za Myanmar, Ufilipino, Vietnam, Bangladesh, Laos, Cambodia, Sri Lanka na Thailand.

Haki miliki ya picha Por Cheng Han
Image caption Adelina alilala sakafunia na mbwa wa mwajiri wake

Mada zinazohusiana