Cyril Ramaphosa ni nani?

Cyril Ramaphosa (L) is hoping to succeed Jacob Zuma (R) as president

Ni mpenda magari yaendayo kwa kasi, mvinyo ulio ghali, ni mvuvi na mkulima - si mwingine ni Cyril Ramaphosa.

Makamu wa raisi wa Afrika Kusini ni mwanasiasa mwenye nguvu na akiwa na utajiri wa kiasi cha dola 450m (£340)

Ramaphosa ni kiongozi mpya wa chama tawala cha Afrika ya kusini African National Congress (ANC), na hii inampa nafasi ya kuwa moja kati ya wagombea urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2019.

Aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa vyama vya ushirika, alikuwa ni alama ya watu weusi katika kukabilina na ubepari kabla ya ANC kuchukua nchi mwaka 1994 na kukomesha utawala wa watu weupe nchini humo.

Baada ya kiongozi wa vyama vya ushirika, alikuwa alama ya uhalifu wa rangi nyeusi huko Afrika Kusini baada ya ANC kuwa na mamlaka mwishoni mwa utawala wa wachache nyeupe mwaka 1994.

Biashara haikuwa kipaumbele chake.

Chaguo lake la kwanza lilikuwa ni siasa na alikuwa na matarajio ya kuwa makamu wa kwanza wa rais Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi nchini Afrika ya kusini.

Mandela alipomkataa kuwa makamu wake alishikwa na hasira na kuamua kutohudhururia kuapishwa kwa Mandela kama rais wa kwanza nchi hiyo. Na pia alikataa kuchukua nafasi yoyote ya uongozi serikalini.

Maelezo ya picha,

Chama cha ANC kimeitawala nchi tangukuisha kwa utawala wa ubaguzi wa rangimnamo 1994

Badala yake, Bwana Ramaphosa ambae pia ni mwanasheria - akajikita kuwa mwakilishi na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba, akiwa na jukumu la kuandaa katiba ya Afrika kusini baada ya kupita kipindi cha miaka mingi ya ubaguzi wa rangi.

Ramaphosa aliwashangaza wananchi wengi wa Afrika Kusini ambao walimwona kama mwanasiasa wa kuaminika zaidi wa kizazi cha baada ya Mandela, aliamua kuachana na siasa na kuwa mfanyabiashara.

Wakati huo, haikuwa kawaida kwa watu weusi, kuwa katika sekta ya biashara iliyokuwa inaongozwa na watu weupe.

Mnamo mwaka 1980 aliandaa mgomo mkubwa wa madini katika historia ya Afrika Kusini.

Wafanyabiashara wenye asili ya weupe walijaribu kumtumikia Bwana Ramaphosa ambae alipata hisa katika karibu kila sekta muhimu - kutoka kwa simu na vyombo vya habari (ambako hakuingilia kati katika uhuru wa wahariri wa magazeti ambayo alikuwa nayo) kwa vinywaji na chakula cha haraka alikuwa anaendesha msururu wa hoteli ya Marekani McDonalds nchini Afrika kusini.

Vibaraka wa kigeni

Bw Ramaphosa daima aliendelea kukiendeleza chama ANC, akiwa kiongozi mkuu wa kamati ya utendaji ya Taifa - nafasi ambayo, wakosoaji wake wanasema ilimpa habari za ndani na akiwa muhudumu wa serikali alitumia nafasi hiyo ya utawala wake kujijenga kibiashara.

Mashtaka haya yalikuja baada ya polisi kuwaua wachimba mgodi 34 wakiwa kazini mwezi wa Agosti 2012 katika mgodi wa Marikana - likiwa ni tukio baya kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizike kwa utawala wa wazungu.

Maelezo ya picha,

Familia za wachimba migodi waliouawa Marikana bado wanadai haki

Ramaphosa akiwa ni mkurungezi wa Lonmin - kampuni ya kimataifa inayomilki mgodi huo - alituhumiwa kwa kuwasaliti wafanyakazi ambao kwa wakti mmoja aliwatetea.

Hususan baada ya kuzuka kwa barua pepe zinazomuonyesha kuwa aliitisha hatua kuchukuliwa dhidi ya wachimba mgodi kwa kushiriki katika 'hatua kali za uhalifu' - akimaanisha mgomo uliokumbwana ghasia ulioshuhudia.

Japokuwa uchunguzi wa hakimu ulimsafisha Ramaphosa na kesi ya mauaji kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighter (EFF) Julias Malema alimwambia Ramaphosa ni kibaraka wa watu weupe.

Hata hivyo, Bwana Ramaphosa, ambae anatajwa na jarida la uchumi la Forbes kuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mwaka 2014 aliamua kuachana na biashara baada ya kuchaguliwa kuwa makamu wa rais.

Gazeti la kifedha la kimataifa la Forbes, lilimnukuu kwamba, "aliachana na shughuli zake za biashara ili kuepuka migogoro ya riba" baada ya kuwa Naibu wa rais wa Afrika Kusini mwaka 2014.

Cyril Ramaphosa kwa kumtupia jicho:

  • Alizaliwa Soweto, Johannesburg, mwaka 1952
  • Mwaka 1974 mpaka 1976 aliwekwa kizuizini kwa shughuli za kupambana na ubaguzi wa rangi.
  • Alianzisha muungano wa kitaifa wa wafanyakazi wa migodi 1982
  • Mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya taifa yaliyoandaa kumpokea Nelson Mandela kutoka gerezani 1990
  • Mbunge na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba wa mwaka 1994
  • Mwaka 1997 aliamua kuingilia kikamilifu biashara kwa muda wote na kuwa moja wa matajiri wakubwa nchini Afrika kusini
  • Alikuwa Katika bodi ya Lonmin wakati wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012
  • Alichaguliwa kuwa makamu wa raisi wa Afrika kusini 2014
  • 2017 alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ANC