Mwanamke aandamana na mkoba wake hadi ndani ya mashine ukaguzi ya X-ray China

Picha ya kanda ya video iliomuonyesha mwanamke huyo akipitia mashine ya X-Ray Haki miliki ya picha PEAR VIDEO
Image caption Picha ya kanda ya video iliomuonyesha mwanamke huyo akipitia mashine ya X-Ray

Je una wasiwasi wa begi lako kutoweka katika eneo la usalama? Mwanamke mmoja wa China aliandamana na begi lake kupitia mashine ya ukaguzi ya X -Ray.

Wafanyikazi katika kituo cha reli cha Kusini mwa China walishangazwa kuona mwanamke huyo akitoka ndani ya mashine hiyo pamoja na begi lake.

Video moja ya mtandaoni ilionyesha kisa hicho cha kushanganza kilifanyika siku ya Jumapili baada ya kuupanda ukanda wa kusukuma mizigo.

Awali mwanamke huyo alitazama begi lake likiwekwa katika mshipi huo na kuondoka.

Tumbili 'waumbiwa' katika maabara China

Nyoka 'watoroka' katika shamba China

Picha za mionzi ya X-Ray zilimuonyesha mwanamke huyo akiwa amepiga magoti nyuma ya begi lake huku akiwa amevaa viatu virefu.

Haijabainika ni kwa nini mwanamke huyo hakutaka kuwa mbali na begi lake ,lakini raia wengi nchini China hubeba kiwango kikubwa cha fedha wakati wanapoelekea nyumbani kusherehekea mwaka mpya.

Haki miliki ya picha PEAR VIDEO
Image caption Abiria huyo aliandamana na mizigo yake kupitia mashine ya X Ray.

Abiria huyo awali alikuwa ameweka begi lake katika ukanda huo wa kusukuma mizigo kabla ya kujaribu kupitia mashine ya ukaguzi akiwa na mkoba wake, picha kutoka kwa kanda za video zilionyesha.

Alielezewa kuwa mabegi yake yote lazima yapitie mashine hiyo ya ukaguzi, lakini akakataa kuuwachilia mkoba wake.

Lengo lake lilikuwa kujiunga na mali yake katika mshipi huo unaosukuma mizigo kabla ya kutoka upande wa pili bila kujali alichokifanya, swala lililomuacha mlinzi mmoja na kicheko.

Wafanyikazi wa kituo hicho cha reli cha Dongguan hatahivyo wamewashauri abiria kutoingia katika mashine za X-Ray kwa kuwa mionzi yake ni hatari kwa mwili wa mwanadamu

Mwanamke huyo ni miongoni mwa takriban watu milioni 390 wanaotarajiwa kusafiri kwa huduma ya treni kwa likizo ya mwaka mpya wa China ambayo itakuwa siku ya Ijumaa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii