Mtoto azaliwa na risasi mwilini nchini Marekani

Mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa wiki 36 wakati alipopigwa risasi. Haki miliki ya picha PA
Image caption Mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa wiki 36 wakati alipopigwa risasi.

Mtoto mmoja amezaliwa na risasi ndani ya mwili wake katika jimbo la Tenesee nchini Marekani.

Mamake mwenye umri wa miaka 19 alipigwa risasi katika kisa kimoja kilichohusisha magari mawili barabarani karibu na mji wa Memphis , kulingana na vyombo vya habari.

Mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa wiki 36 wakati alipopigwa risasi.

Alipelekewa hospitalini ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na ndiposa akajifungua mwanawe.

Mtoto huyo alizaliwa na majeraha akiwa katika hali mahututi, kulingana na maafisa wa polisi wa Memphis.

Mwanamume aliyeandamana na mwanamke huyo hospitalini aliambia maafisa wa polisi kwamba watu watatu waliokuwa katika gari jeusi aina ya Chevrolet walikaribia gari lao barabarani kabla ya kuwafyatulia risasi kulingana na chombo cha habari cha Fox 2 News.

Mama huyo alipigwa risasi mara tatu katika nyonga yake ya kulia, kituo hicho kiliripoti

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii