Trump lawamani na sheria ya silaha

Shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouwawa Haki miliki ya picha Joe Raedle
Image caption Shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouwawa

Chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.

Hii imetokea siku moja baada ya wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani.

Wakati huo huo shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouawa kwenye tukio hilo imefanyika huko Florida kulikotokea tukio hilo.

Wakati wa Marekani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza kifo cha wanafunzi 17 waliuawa kwa kupigwa risasi kumekuwa na wito wa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha.

Haki miliki ya picha Win McNamee
Image caption Rais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya shambulio

Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele.

Hata hivyo alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha.

"Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za eneo la mji kuchunguza tukio la kupigwa risasi na kupata taarifa zote iwezekanavyo. Tumejitolea kufanya kazi na jimbo pamoja na viongozi wa eneo hilo kusaidia kulinda usalama wa shule na kukabiliana na masuala magumu yanayotokana na matatizo ya afya ya akili." alisema Rais Trump

Siku ya Jumatano watu 17 waliuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi aliyefukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu katika shule moja huko katika jimbo la Florida.

Haki miliki ya picha AFP/ GETTY IMAGES
Image caption Wanafunzi 3000 wa shule hio walikuwa wanamalizia siku yao wakati shambulio hilo lilipotokea

Akihutubia katika tukio hilo Baba wa mwanafunzi wa miaka 14 aliyeuawa kwenye tukio hilo Fred Guttenberg amesema familia yake imeumia kutoka na kifo mtoto wao.

"Haina maana. Hii haiwezekani. binti yangu , mtoto wangu mwenye umri wa miaka 14. na kwenu mnaojua binti yangu Jamie, alikuwa ni maisha katika burudani. Alikuwa anatutia nguvu tukio nyumbani.

Haki miliki ya picha Pool
Image caption Mtuhumiwa huyo akifika mbele ya mahakama kusikiliza mashtaka