Wasifu wa marehemu Morgan Tsvangirai

Morgan Tsvangirai Haki miliki ya picha Getty Images

Nguvu yake kubwa ilikuwa ujasiri wake, alihatarisha maisha yake kusimama dhidi ya utawala wa Robert Mugabe na washirika wake ndani ya vikosi vya usalama.alipigwa vibaya mara mbili na kushtakiwa mara tatu kwa kosa la uhaini.

Hata hivyo, alikuwa akijikuta anazidiwa ujanja na Robert Mugabe ambaye alikataa kutoka madarakani

Tsvangirai hatimaye aliapishwa kuwa waziri mkuu lakini ilishindikana kwake kufanya mabadiliko yeyote.Hata hivyo alishiriki katika harakati za kumuangusha Mugabe mwaka 2017.

Morgan Richard Tsvangirai alizaliwa tarehe 10 mwezi Machi mwaka 1952 eneo liitwalo Gutu Rhodesia ya kusini,akiwa mmoja kati ya watoto tisa wa fundi seremala.

Aliacha shule na kuwa mfumaji wa nguo, lakini baadae alikwenda kufanya kazi mgodini mjini Bindura, maiali hamsini kutoka Kaskazini mashariki mwa Harare.

Tsvangirai akajihusisha na harakati za vyama vya wafanyakazi na akachaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa mgodini.

Zimbabwe ilipopata uhuru mwaka 1980 alijiunga na chama cha Mugabe, Zanu PF na kushika nafasi ya afisa wa juu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tsvangirai alijifunza namna ya kupiga kampeni katika migodi ya shaba Rhodesia

Mwishoni mwa miaka ya 1980, alikuwa Kiongozi wa jumuia ya wafanyakazi nchini Zimbabwe.

Chama hicho kilipoanza kuvunja uhusuano wao na Zanu-PF Tsvangirai akawa Kiongozi wa kundi la upinzani lenye nguvu

Mwezi Desemba mwaka 1997, aliongoza mfululizo wa migomo iliyojulikana kama ''Stayaways'', dhidi ya ongezeko la kodi, ambayo iliwaacha watu kwenye taharuki kubwa.

Hatua hiyo ililazimu serikali ya Mugabe kufuta ongezeko la kodi mbili na kodi ya kusaidia pensheni ya maveterani wa kivita

Katika hali ya kulipa kisasi kwa ajili ya maveterani hao, kundi la wanaume walivamia Ofisi ya Tsvangirai wakampiga na chuma kichwani na kujaribu kumtupa nje kupitia dirisha la ghorofa la kumi.

Hakuwa na mtangulizi

Mwaka 1999 Tsvangirai alianzisha Chama cha Democratic Change (MDC), kilichovutia kizazi cha vijana wa Zimbabwe, hasa wafanyakazi wa mijini.

Hawakuvutwa sana na historia ya Mugabe kama muasisi wa taifa hilo bali namna ambavyo uchumi wa taifa hilo ulivyokuwa ukiyumba.

Ndani ya miezi kadhaa , chama kipya kilisaidia kuishinda serikali kwenye kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba, ambayo ilikuwa na vifungu vinavyoruhusu kuzuia mashamba yanayomilikiwa na watu weupe bila kulipwa.

Katika uchaguzi wa mwaka 2000, chama chake kilipunguza makali ya chama tawala kwa kuzoa viti 57 vya ubunge dhidi ya 62 vya Zanu-PF

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption The 2000 election saw the MDC threaten Mugabe's stranglehold on power

Mgawanyiko

Mwaka 2001 Tsvangirai alitoa hotuba ya kukemea mauaji ya waasi waliokuwa wakimpinga Mugabe katika mji wa Matabeleland mwaka 1984, ambapo takriban watu 20,000 walipoteza maisha.

Katika hotuba yake aliahidi waliohusika watapelekwa mbele ya vyombo vya haki na kuwa MDC ilipaswa kuwa madarakani.

Alikamatwa tena mwaka 2003 baada ya kuongea na wanahabari akimshutumu Mugabe kutishia na kuendelea kung'ang'ania madarakani.

Maafisa ndani ya MDC wamejikuta wakisigana mwaka 2005, huku baadhi ya wanachama akiwemo Tsvangirai ,akitoa wito wa kususia uchaguzi mpaka pale itakapojihakikishia kuwa kura hizo zitakapokuwa huru na haki.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tsvangirai hawakuwa na kinga dhidi ya ghasia ambazo zilielekezwa kwa wapinzani wa serikali

Matokeo ya mgawanyiko huo yalileta matokeo mabaya katika uchaguzi wa maseneta, MDC ikinyakua viti vitano pekee kati ya 60.

Pamoja na kuwepo kwa mgogoro wa ndani, Chama hicho kiliendelea kujizolea umaarufu na kuungwa mkono ,kikielezwa kuwa tishio kubwa kwa Mugabe.

Mwaka 2007 Tsvangirai alikamatwa tena na wakati huu alipelekwa kwenye kambi ya vikosi maalum ambapo kwa saa kadhaa alipigwa vibaya, na kusababisha majeraha kwenye fuvu lake na kuvuja damu kwa ndani.

Kuanganishwa tena

Wiki kadhaa baada ya kupigwa ,polisi walivamia makao makuu ya MDC kwa mara nyingine Tvangirai alikamatwa.

Tarehe 29 mwezi Machi MDC ikiwa imegawanyika, uchaguzi wa urais na wabunge ulikuwa ukifanyika nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi wa uraisi yalicheleweshwa kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuwepo shutuma kuwa serikali ilikuwa inajaribu kuiba kura.

Baada ya kuhesabu tena, tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe ilisema hakuna mgombea aliyefikisha asilimia 50 kama ilivyokuwa ikitakiwa kuwa hivyo na kuitisha duru ya pili ya uchaguzi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Japo anatabasamu Mugabe hakuwa na nia ya kugawana madaraka

Tsvangirai alifurahishwa na taarifa kuwa MDC ilijizolea viti vingi vya ubunge, awali aliridhia kushiriki uchaguzi wa duru la pili.

Lakini kampeni zake zilikabiliwa na changamoto ,vitisho na ghasia, huku mikutano ya MDC ikishambuliwa na wafuasi wakipigwa hata kuuawa.

Siku kadhaa kabla ya uchaguzi alijitoa kwenye mchakato huo akisema kuwa haiwezekani uchaguzi huo ukawa huru na haki akimuacha Mugabe kuwa mgombea pekee.

Mwezi Julai mwaka 2008 alikutana na Mugabe kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa ukiwa mwanzo wa uwezekano wa kuwa na serikali ya mseto.

Hatimaye Tsvangirai aliapishwa kuwa Waziri Mkuu.

Tsvangirai alikumbana na ukosoaji mkali kutoka kwenye chama chake ambapo kilidai uamuzi wake wa kuwa na serikali ya pamoja umeruhusu Mugabe aendelee kubaki madarakani.

Matokeo yake ilikuwa kupotea kwa imani na uongozi wa Tsvangirai, hatimaye MDC ilishindwa vibaya katika uchaguzi wa mwezi julai mwaka 2013.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chama cha MDC walishindwa katika uchaguzi wa 2013

Miezi miwili baadae Tsvangirai alijiuzulu uwaziri mkuu, hata hivyo alikuwa na ujasiri wa kupambana na vitisho na kuwapa matumaini raia wa kawaida wa Zimbabwe kuwa siku zote kuna mbadala wa utawala wa Mugabe.Hatimaye alishuhudia kuanguka kwa utawala wa Mugabe , jambo alilopambana kulifanikisha kwa muda mrefu.

Mada zinazohusiana