Aliyemtunuku Grace Mugabe shahada ya uzamifu akamatwa Zimbabwe

Bi Grace Mugabe Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bi Grace Mugabe

Naibu chansela wa chuo kikuu cha Zimbabwe amekamatwa kuhusiana na utoaji wa wa cheti cha shahada ya uzamifu kwa mke wa rais wa zamani nchini humo Robert Mugabe.

Grace Mugabe alitunukwa cheti hicho baada ya kusoma kwa miezi michache na hoja yake ikachapishwa mwezi uliopita baada ya kuzuka kwa wito wa kupokonywa shahada hiyo

Tume ya uchaguzi inatarajiwa kumshtaki naibu huyo Levi Nyagura kwa utumizi mbaya wa ofisi.

Kile ambacho hakiko wazi ni iwapo bi Mugabe atakamatwa.

Badala ya kusoma miaka kadhaa alipokea shahada yake miezi kadhaa baada ya kusajiliwa katika chuo hicho.

Alikuwa akijaribu kuwa rais wa taifa hilo lakini baada ya jeshi kumuondoa madarakani Robert Mugabe mwezi Novemba harakati zake za kisiasa ziligonga mwamba hatua iliowafurahisha raia wengi wa Zimbabwe.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii