Wanajeshi wa Israel washambuliwa kwa bomu karibu na mpaka na Gaza

Israeli soldiers stands near a military jeep next to the border fence with the southern Gaza Strip near Kibbutz Nirim, Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Israel washambuliwa kwa bomu karibu na mpaka na Gaza

Wanajeshi wa Israel wamejeruhiwa wawili kati yao vibaya wakati wa mlipuko karibu na mpaka wa Israel na Ukanda wa Gaza.

Jeshi lilisema kuwa bendera ya palestina ilikuwa ikipepea eneo hilo, na wakati wanajeshi walikaribia wakakumbwa na mlipuko.

Israel iliendesha mashambulizi ya ndege katika vituo vya kundi la Hamas kujibu.

Katika kisa tofauti vijana wawili wa kipalestina waliuawa kwa risasi zilofyatuliwa kutoka kusini mwa Rafah nchini Israel.

Wawili hao walikaribia mpaka kwa njia ambayo ilitiliwa shaka, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

Israel na wanamgambo wa Hamas ambao wamethibiti ukanda wa Gaza walipigana vita mwaka 2014.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na mlipuko huo wa siku ya Jumamosi ambao ulitokea kusini mwa mji wa Khana Younis

Image caption Wanajeshi wa Israel washambuliwa kwa bomu karibu na mpaka na Gaza

Jeshi lilisema kwa mlpuko ulikuwa umetegwa enoo hilo wakati wa maandamano ya siku ya Ijumaa na ulikuwa umeiunganishwa kwa bendera ya palestina.

Jeshi la Israel lilisema kuwa lililenga vituo 18 vya Hamas kuanzia Jumamosi usiku hadi Jumapili kkiwemo kiwanda cha kuunda silaha na barabara za chini kwa chini zinazochimbwa na wanamgambo.

Maafisa wa kipalestina walisema kuwa kambi tatu za mafunzo ya Hamas na moja ya kundi dogo zilishambuliwa.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa roketi iliyofyatuliwa kutoka Gaza ilianguka kusini mwa nchi Jumamosi jioni.

Mada zinazohusiana