Watu wote 66 waangamia kwenye ajali ya ndege Iran

ATR 72-500 Haki miliki ya picha Konstantin von Wedelstaedt
Image caption Ndege ya Aseman ya ATR 72-500

Watu 66 wameuawa kwenye ajali ya ndege ya abiria nchini Iraan, maafisa wa kampuni wamesema.

Ndege hiyo ya shirika la Aseman, ilikuwa safarini kutoka mjini Tehran kwenda mji wa kusini magharibi wa Yasuf wakati ilianguka kwenye milima ya Zagros kati kati mwa Iran.

Shirika la msalaba mwekundu lilituma kikisi cha uokoaji kweda eneo hilo karibu na mji wa Semirom mkoa wa Isfahan.

Ndege hiyo namba 3704 iliondoka Tehran mwendo wa saa (01:30 GMT) na kutoweka kutoka kwa rada baadaye.

Maafisa wanasema kuwa hali mbaya ya hewa imetatiza jitihada za uokoaji.

Ndege hiyo inaaminiwa kuwa ya miaka 20 iliyotengenezewa nchini Ufaransa.

Ripoti zinasema kuwa wale waliokuwa ndani ya ndege ni abiria 60, walinzi wawili, wahudumu wawili, rubani na msaidizi wake.

Image caption Ramani

Mada zinazohusiana