Wafungwa wachukua udhibiti wa gereza mjini Rio de Janeiro, Brazil

Wafungwa wachukua udhibiti wa gereza mjini Rio de Janeiro Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafungwa wachukua udhibiti wa gereza mjini Rio de Janeiro

Wafungwa wamechukua udhibiti wa gereza kwenyr mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil na wanawashika mateka baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo.

Polisi waliojihami wanalizunguka gereza hilo lenye msongamano wa wafungwa la Japari ambalo liko chini ya udhibiti wa genge moja la wahalifu lenye guvu nyingi mjini humo.

Wafungwa watatu ambao walihusika katika kulidhibiti gereza hilo wamepigwa risasi lakini hawajapa majeraha ya kuwatishia maisha.

Ghasia hizo zinatokea siku mbili baada ya Rais wa Brazil Michel Temer, kusaini sheria ya kuwapa wanajeshi ruhusa ya kusimamia usalama wa mji wa Rio de Janeiro.

Maafisa wa gereza wanasema ghasia hizo huenda zimechangiwa na hatua mpya za ulinzi.

Mada zinazohusiana