Kwa Picha: Maisha baada ya janga la Ebola Afrika Magharibi

Imekuwa ni miaka minne tangu utokee mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola kwenye mataifa ya Magharibi mwa Afrika ya Liberia, Guinea na Sierra Leone. Mpiga picha Hugh Kinsella Cunningham amerudi kufuatilia jinsi watu wanavyoishi tangu ugonjwa huo uangamizwe

An aerial view of West Point, Monrovia, Liberia. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption West Point, Monrovia, Liberia.

Mlipuko huo wa mwaka 2014 ulisabisha vifo vingi zaidi kulika milipuko mingine yote ya ebola kwa jumla, tangu virusi vya ugonjwa huo vigunduliwe mwaka 1976.

Virusi hivyo viliathiri maeneo maskini kama West Point nchini Liberia.

West Pointi ni eneo lenye watu wengi huko Monrovia. Wakati serikali ilitangaza amri ya kutotembea na kulizingira eneo hilo kama njia ya kuzuia kusamba kwa ugonjwa huo ghasia zilizuka.

Eva Nah pictured outside her house in West Point, Monrovia, Liberia. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Eva Nah

Mjuu wake Eva Nah aliuawa na polisi wakati akiandamana kupinga hatua hiyo ya serikali. "Mama na baba yake walikufa kwa hivyo ni mimi nilikuwa nikimhudumia," alisema Eva.

Miaka kadhaa baadaye, fidia ya serikali kutokana na kuuliwa kwake imemwezesha Eva kuwasomesha watoto wengine kwenye familia.

Rita Carol alimpoteza dada yake. Alikuwa akiuza chakula kwenye barababara za West Point lakini ameweka akiba pesa za kutosha kuanza biashara yake.

Rita Carol in her home in West Point, Monrovia. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Rita Carol
Etta Roberts works as a nurse at the Kahweh clinic. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Etta Roberts

Etta Roberts anafanya kazi kama muuguzi kwenye zahanati ya Kahweh, iliyo mashariki mwa Monrovia. Kawaida huwatibu wagonjwa 10 kwa siku kwa ugonjwa wa Malaria.

Mwanzilishi wa kliniki Reginald Kahweh, aligharamia jengo hilo baada ya kuwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa Ebola. Kila mtu ni lazima ahakikishe kuwepo kwa jamii bora...eneo hilo limebuniwa kuwakumbuka wale waliokufa.

A doctor at the West Point medical clinic. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Daktari katika zahanati ya West Point

Ugonjwa wa Ebola ulikuwa pigo kwa mfumo wa afya nchini Liberia ambapo uliilemea kwa haraka. Miundo msingi ya nchi hiyo ilikuwa tayari imeharibiwa na vita vya miaka 14 vya wenye kwa wenyewe na mifumo ya afya ilikuwa na wakati mgumu kutekeleza majukumu ya kawaida.

Swamps in Bong County, Liberia. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Liberia
J Roberts in his washing facility Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption J Roberts

J Roberts anaishi enoe lililo karibu na bahari la West Point. Baada ya kumpoteza mke wake kwa ugonjwa wa Ebola alianzisha biashara. Mke wangu alichomwa badala ya kuzikwa kwa hivyo ninahisi kama alienda kabisa. Niliamua kuwalea watoto wetu wanne," anasema.

Cross on a hill in Waterloo district, Sierra Leone. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Mbele ya mlima wilaya ya Waterloo, Sierra Leone.

Wafanyakazi wengi waliofanya kazi ya kuzika waathiriwa wa Ebola nchini Sierra Leone walikuwa ni masiki na walipata fursa hiyo kwa sababu hawakuwa na kazi.

Waterloo Ebola Graveyard. Sierra Leone. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Makaburi ya waathiriwa wa Ebola ya Waterloo Sierra Leone.
Mohammed Kanu, a former frontline worker during the Ebola crisis at Waterloo Ebola Graveyard. Sierra Leone. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Mohammed Kanu

Mohammed Kanu aliajiriwa na sarikali kuzika miili wakati wa Ebola, hajapata kazi nyingine na amebaki akitunza makaburi kwa mshahara kidogo.

A graveyard worker with his back to the camera walks through Waterloo Ebola Graveyard. Sierra Leone. Haki miliki ya picha Hugh Kinsella Cunningham
Image caption Makaburi ya Waterloo ,Sierra Leone.

Picha zote haki miliki Hugh Kinsella Cunningham.

Mada zinazohusiana