Mpigapicha wa wanyamapori ashinda tuzo la 'People's Choice'

Picha ya kusisimua ya sokwe na mmoja wa waokoaji wake imeshinda tuzo la mpigapicha bora wa mwaka la Chaguo la Watu au 'People's Choice'

Haki miliki ya picha Jo-Anne McArthur / Natural History Museum
Image caption Sokwe pichani akiwa na muokoaji wake Appolinaire

Picha hii iliyoshinda tuzo la mwaka ilichukuliwa na mpigapicha wa Canada, Jo-Anne McArthur ilionesha sokwe huyo mdogo, kutoka eneo la nyika Tambarale ambaye aliokolewa na kampuni ya Ape Action Africa kutoka kwa wawindaji haramu.

Katika picha hii anaonekana kwenye mikono ya mchungaji wake, Appolinaire Ndohoudou, wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka kwenye makazi madogo ya sokwe hadi kwenye makao salama ya msitu wa Cameroon, ambako kuna msitu mpana zaidi.

"'Ninashukuru sana kwamba picha hii imewagusa watu na ninatumai inaweza kutufundisha sote kuwajali walau kidogo wanyama," anasema McArthur. "Hakuna kitendo chochote cha ukarimu kwao kinachokua kidogo sana"

"'Mara kwa mara ninarekodi ukatili wanaopitia wanyama katika mikono yetu, lakini wakati mwingine ninashuhudia taarifa za uokozi, matumaini na ukombozi wao."

Picha hii ilichaguliwa takriban mara 20,000 na mashabiki wa mazingira kutoka kwenye orodha ya picha 24 zilizochaguliwa na makavazi ya kihistoria ya mali asili, ambazo zilichaguliwa kati ya picha from takriban 50,000 zilizowashilishwa kwa ajili ya shindano la kuwania tuzo la picha bora ya mwaka 2017.

Picha nyingine zilizoweza kufika finali ni zifuatazo:

Haki miliki ya picha DEBRA GARSIDE / Natural History Museum
Image caption Familia ya dubu

Mama wa dubu wametoka kwenye makao yao wakati wa majira ya joto huku watoto wao wakiwakumbatia ili kupata joto na ulinzi. Mpiga picha Debra Garside alisubiri kwa muda wa siku sita karibu na familia hii ya dubu ili kuichukua picha hii, katika mbuga ya wanyama ya Wapusk National Park, Manitoba, nchini Canada. Hali ya hewa ilikua mbaya ambapo vipimo vya joto vilikua kati ya nyuzi joto -35 C (-31 F) hadi -55 C (-67 F) na upepo mkali, lakini Garside alivumilia na kufanikiwa kuchukua picha hii.

Haki miliki ya picha Lakshitha Karunarathna / Natural History Museum
Image caption Ndege akiwa juu ya mgongo wa pundamilia

Lakshitha Karunarathna alikua katika safari ya utalii katika mbuga ya wanyama ya taifa nchini Kenya ya Maasai Mara National, alipoona picha ya ajabu - ndege wa kuvutia akiwa juu ya mgongo wa pundamilia aliyekua akitembea. Ndege mwenye rangi za kuvutia alidandia kwenye mgongo wa pundamilia kwa muda wa saa nzima au zaidi akiendeshwa na wakati mwingine kula kwa starehe wadudu aliowaokota huku na kule. Karunarathna alisubiri kwa muda hadi pundamilia wengine waliokuwa wamemzungira pundamilia huyo walipompatia fursa ya kuchukua picha hii kwa ukaribu zaidi.

Haki miliki ya picha Luciano Candisani / Natural History Museum
Image caption Mnyama aina ya 'sloth' akikwea tawi la mtu katika msitu wa Atlantiki unaolindwa kusini mwa Bahia, Brazil

Mpiga picha Luciano Candisani alilazimika kukwea mti aina ya Cecropia, katika msitu wa Atlantic unaolindwa kusini mwa Bahia, Brazil, kuchukua picha hii ya usawa wa macho ya aina ya nyani huyu aitwaye 'Sloth' . Mnyama huyu wa ajabu ana miguu mitatu . Nyani huyu hupenda kula majani ya matawi hii ya miti na mara nyingi huonekana kwenye matawi ya juu zaidi ya miti hii.

Shindano la kuwania tuzo la mpigapicha bora wa makavazi ya historia asilia hufanyika kila mwaka ambapo picha bora ya mnyama na uandishi wa habari za wanyamapori hutangazwa.

Tarehe 28 Mei, 2018 atatangazwa mshindi wa tuzo ya picha bora ya wanyamapori katika onyesho la picha hizo jijini London.

Mada zinazohusiana