Trump 'aunga mkono' uboreshaji wa ukaguzi wa silaha

US President Donald Trump (R) speaks with Broward County Sheriff Scott Israel Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Rais Trump aliwatembelea wahanga na mamlaka waliohusika na shambulio Florida wiki iliyopita

Rais wa Marekani Donald Trump "anaunga mkono" jitihada za kuboresha ukaguzi wa manunuzi wa wamiliki silaha, Ikulu ya Whitehouse imesema.

Taarifa imesema amezungumza na Seneta wa chama cha Republican John Cornyn kuhusu mswada wa vyama viwili alioiwasilisha.

Mswada huo wa mwaka 2017 unalenga kuboresha vibali vya serikali ya shirikisho vitakavyopitshiwa kabla ya mtu kununua bastola.

Hii inakuja baada ya mamlaka kusema kuwa mtuhumiwa katika shambulio ya shule jimboni Florida alinunua silaha ya kihalali.

Shirkia la taifa la Ukaguzi wa Uhalifu kwa sasa unategemea maafisa wa jimbo na serikali kuu kuripoti mtu yeyote mwenye historia ya uhalifu au mwenye matatizo ya akili anayejaribu kununua silaha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanafunzi wakiokolewa

Udhaifu wake uligundulika mwaka jana baada ya kikosi cha anga cha Marekani walikubali kwamba walikosa kuchukua hatua dhidi ya mshambuliaji mwenye historia ya uhalifu kabla alipowapiga risasi na kuwaua watu 27 katika kanisa la Sutherland Springs, Texas.

Baada ya shambulio hilo, mswaha huo wa vyama viwili uliwasilishwa na Bw Cornyn na Senata wa Demcrats Chris Murphy.

Msimamo wa Bw Trump juu ya udhibiti wa silaha umebadilika mara kwa mara, lakini aliwania rais kama mgombea anayepinga udhibiti wa silaha mwaka 2016

Mwaka jana Rais aliwaambia shirika la taifa la silaha ,NRA kwenye mkutano kuwa "hangewahi kabisa kuingilia" haki za kikatiba ya umiliki silaha.

Awali alilaumu FBI na hali ya afya ya kiakili ya mshambuliaji kwa shambulio ya shule huko Florida lakini hakutoa tamko lolote kuhusu wito mpya wa wanafunzi kudhibiti silaha.

Mada zinazohusiana