BBC yaanzisha idhaa kwa lugha za Igbo na Yoruba nchini Nigeria

Members of the BBC Igbo and Yoruba teams in Lagos, Nigera
Image caption Kuna machapisho ya habari chache kwa wazungumzaji wa Igbo na Yoruba

Idhaa mpya mbili zimezinguliwa na idhaa ya BBC kwa ajili ya wazungzaji wa Yoruba na Igbo nchini Nigeria na Afrika Magharibi na Kati.

Maadhui yao ya kidigitali ni kwa ajili wa watumiaji wa simu za mkononi.

Lugha ya Igbo inazungumzwa haswa kusini-mashariki ya Nigeria na Yoruba inazungumzwa pia nchini Benin na Togo.

Idhaa hizi mpya ni sehemu ya upanuzi wa idhaa ya dunia tangu miaka ya 1940 kufuatia ongezeko wa ufadhili kutoka serikali ya Uingereza mwaka uliotangazwa mwaka 2016.

Kwa ujumla, idhaa 12 zitazinduliwa na BBC barani Afrika na Asia.

Mambo saba kuhusu lugha ya Igbo

 • Mzungumzaji mashuhuri alikuwa Chinua Achebe, anayechukuliwa kuwa baba mwanzilishi wa fasihi Afrika
 • Inakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 30, hasa kutoka kusini mashariki ya Nigeria
 • Neno moja yenye maandishi sawa yaweza kuwa na maan tofauti kwa mfano neno "akwa" ni yai, kitanda, kitambaa - yote inategemea na matamshi ya neno hilo
 • Wimbi wa kujitenga kutoka Waigbo ulianzisha vita hatari ya ndani kwa ndani mwaka 1967
 • Karanga ya Kola yenye kafeini ni sehemu muhimu katika utamaduni ya Igbo - inatumiwa kuwakaribisha wageni
 • Msemo maarufu: "Onye wetara ọjị, wetara ndụ" kumaanisha "Yule anayeleta kola, analeta maisha"
 • bbc.com/igbo pia ipo Facebook na Instagram

Kutana na timu ya BBC Igbo:

Upanuzi wa BBC nchini Nigeria - nchi yenye idadi wengi ya watu barani Afrika ambako zaidi ya lugha 200 zinazungumwa -ulianzia mwaka jana kwa idhaa ya BBC Pidgin, ambayo iliwalenga wazungumzaji wanaozungumza lugha ya kiingerezayenye mchanganyiko na kifaransa.

Ni lugha ya maongezi kimsingi, isiyokuwa na uandishi rasmi uliokubaliwa.

Kikosi cha Idhaa ya BBC Igbo na Yoruba kimekumbana na changamoto ya kuweka kiwango cha uandishi wa lugha hizo kwa hadhira za kisasa d - and have sought advice from academics na zimepata ushauri kutoka kwa wasomi.

"Lugha ya Yoruba inaweza kuwa yenye mkanganyiko sana kwa wasomaji vijana kwasababu maneno yake yana mfumo tofauti wa maana zake, kwa hiyo tunatumia mfumo ambao sio mgumu kuwavutia ," anasema mhariri wa idhaa ya Yoruba Temidayo Olofinsawo.

Mambo muhimu kuihusu lugha ya Yoruba

 • Mzungumzaji wake maarufu ni Wole Soyinka, mshindi wa tuzo ya Nobel mwandishi wa maigizo na ushairi
 • Ina wazungumzaji zaidi ya milioni 40 ,hususan kusini magharibi mwa Nigeria
 • Neno lenye herufi swa linaweza kuwa na maana tofauti, kwa mfano neno "owo" ni pesa, heshima, mkono ama ufagio...inategemea na sauti ya namna lilivyotamkwa
 • Watu wengi ni wafuasi wa dini ya kitamaduni ya Yoruba Amerika Kusini na Caribbean kuliko Nigeria - kutokana na biashara ya utumwa kupitia Atlantiki
 • Filamu za Yorubana muziki wake vimeboresha sekta ya filamu za kiNigeria -Nollywood
 • Msemo maarufu wa Yoruba ni ule usemao: "Ile laawo k'a to s'ọmọ lorukọ" ikimaanisha : "Unapaswa kumuita mwanao jina kulingana na maisha yanyuma ya familia yako ".

Meet the BBC Yoruba team:

Kuna taarifa chache za habari zilizokwisha chapishwa katika lugha za Igbo na Yoruba nchini Nigeria,kwa hiyo ni matumaini kwamba idhaa hizi mpya za BBC zitakuwa maarufu kwa waNigeria wa nyumbani na waliopo ugaibuni.

" Hii itakua mara ya kwanza kwa lugha ya Igbo kuandikwa na kutangazwakwa ajili ya umma wakimataifa ," anasema Adline Okere, mhariri wa Idhaa ya Igbo.

" Wa Igbo wanafahamika kwa moyo wa ujasiliamali - na wameenea kote duniani ," anasema.

Watafanya nini

Watangazaji watatangaza wa idhaa hizi watatangaza taarifa za habari mara mbili kwa siku kupitia BBC - ambapo watatangaza taarifa za ripoti pamoja na habari, uchambuzi na maeleo , pamoja na habari za kwenye mtandao wa internet pamoja na mitandao ya kijamii.

Image caption Kikosi cha watangazaji wa BBC Yoruba kikiwa pamoja na Profesa wa Lugha wakikamilisha mtindo na sarufi ya lugha

Mkuu wa BBC kanda ya Afrikamagharibi, Oluwatoyosi Ogunseye,anasema malengo yatakuwa ni kupata taarifa za uandishi asilia .

"Kuwasilisha ujumbe na kuwahusisha wasikilizaji wa lugha za Igbo na Yoruba katika lugha yao mama , inasisimua na kufurahisha," anasema

"Tumekua na BBC Hausa [lugha ambayo zaidi inazungumwa kaskazini mwa Nigeria] kwa miongo na tumeona athari ambayo imekuwa nayo kwa hadhira yake.

"Tukiitizama Nigeria tuna jamii yenye tamaduni nyingi na BBC ilihisi kuwa ni muhimu kuzipatia tamaduni zote fursa ya kuwasiliana na kukutana ."

Image caption Lugha mpya zinazotarajiwa kutangazwa katika Idhaa ya dunia ya BBC

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC