BBC yaanzisha idhaa kwa lugha za Igbo na Yoruba nchini Nigeria

Members of the BBC Igbo and Yoruba teams in Lagos, Nigera
Image caption Kuna machapisho ya habari chache kwa wazungumzaji wa Igbo na Yoruba

Idhaa mpya mbili zimezinduliwa na idhaa ya BBC kwa ajili ya wazungumzaji wa Yoruba na Igbo nchini Nigeria na Afrika Magharibi na Kati.

Maadhui yao ya kidigitali ni kwa ajili ya watumiaji wa simu za mkononi.

Lugha ya Igbo inazungumzwa haswa kusini-mashariki ya Nigeria na Yoruba inazungumzwa pia nchini Benin na Togo.

Idhaa hizi mpya ni sehemu ya upanuzi wa idhaa ya dunia tangu miaka ya 1940 kufuatia ongezeko wa ufadhili kutoka serikali ya Uingereza mwaka uliotangazwa mwaka 2016.

Kwa ujumla, idhaa 12 zitazinduliwa na BBC barani Afrika na Asia.

Mambo saba kuhusu lugha ya Igbo

 • Mzungumzaji mashuhuri alikuwa Chinua Achebe, anayechukuliwa kuwa baba mwanzilishi wa fasihi Afrika
 • Inakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 30, hasa kutoka kusini mashariki ya Nigeria
 • Neno moja yenye maandishi sawa yaweza kuwa na maan tofauti kwa mfano neno "akwa" ni yai, kitanda, kitambaa - yote inategemea na matamshi ya neno hilo
 • Wimbi wa kujitenga kutoka Waigbo ulianzisha vita hatari ya ndani kwa ndani mwaka 1967
 • Karanga ya Kola yenye kafeini ni sehemu muhimu katika utamaduni ya Igbo - inatumiwa kuwakaribisha wageni
 • Msemo maarufu: "Onye wetara ọjị, wetara ndụ" kumaanisha "Yule anayeleta kola, analeta maisha"
 • bbc.com/igbo pia ipo Facebook na Instagram

Kutana na timu ya BBC Igbo:

Upanuzi wa BBC nchini Nigeria - nchi yenye idadi wengi ya watu barani Afrika ambako zaidi ya lugha 200 zinazungumzwa- ulianzia na BBC Pidgin, ambayo iliwalenga wazungumzaji wanaozungumza lugha zenye misingi ya kiingereza na kifaransa.

Ni lugha ambayo kimsingi ni ya kuongea, ikiwa haina kiwango rasmi cha mfumo wa uandishi kilichokubalika.

Waandishi wa Idhaa za BBC Igbo na Yoruba pia walikabiliwa na changamoto ya kuweka kiwango cha uandishi wa lugha hizi kwa hadhi ya juu - na walipata ushauri wa wasomi.

"Yoruba ni lugha inayoweza kuwakanganya hasa wasomaji vijana kwa sababu ya kuwa na maneno yenye maana tofauti kwa hiyo tunatumia mfumo rahisi kuwavutia," anasema mhaririri wa Idhaa ya Yoruba Temidayo Olofinsawo.

Mambo saba kuihusu lugha ya Yoruba

 • Mzungumzaji anayefahamika zaidi wa Yoruba ni Wole Soyinka, mshindi wa tuzo ya Nobel mwandishi wa maigizo na ushairi
 • Zaidi ya watu milioni 40 wanazungumza Yoruba, wengi wao wanaishi Kusini magharibi mwa Nigeria
 • Neno lenye herufi zinazofanana linaweza kuwa na maana tofauti, kwa mfano "owo" ni pesa, heshima, mkono ama mfagio- inategemea na sauti unayotumia kulitamka
 • Watu wengi zaidi ni wafuasi wa dini ya kitamaduni ya Yoruba Amerika Kusini na Caribbean kuliko Nigeria - kutokana na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki
 • Filamu za Yoruba na tasnia ya muziki vimeimarisha sekta ya filamu ya Nollywood
 • Methali maarufu katika lugha hii ni ule usemao: "Ile laawo k'a to s'ọmọ lorukọ" ikimaanisha: "Jina unalomuita mwanao halinabudi kuwa na taswira ya maisha yaliyopita ya familia yako''
 • bbc.com/yoruba iko pia katika Facebook na Instagram

Kutana na timu ya watangazaji wa Yoruba:

Kuna taarifa chache sana zilizokwisha chapishwa kwa lugha za Igbo na Yoruba nchini Nigeria kwa hivyo ni matumaini kuwa idhaa hizi mpya za BBC zitakuwa maarufu miongoni mwa Wanigeria wa ndani na ughaibuni.

"Hii itakua ni mara ya kwanza kwa lugha ya Igbo kuandikwa na kutangazwa kwa ajili ya wasikilizaji wa kimataifa," anasema Adline Okere mhariri wa Idhaa ya Igbo.

"WaIgbo wanafahamika kwa moyo wao wa ujasiliamali - na wameenea kote duniani," anasema.

Watatoa huduma gani?

Kikosi kitazalisha taarifa za habari mara mbili kwa siku - na taarifa hizi zitakuwa na ripoti za sauti pamoja na habari, uchambuzi, maelezo, na taarifa za kina kwenye tovuti na mitandao ya kijamii.

Image caption Kikosi cha waandishi wa idhaa ya BBC Yoruba kikiwa pamoja na profesa wa lugha wakijadiliana kuhusu mtindo na sarufi

Mkuu wa BBC kanda ya Afrika Magharibi, Oluwatoyosi Ogunseye, anasema leo, lao litakua ni kutoa taarifa za uandishi asilia.

"KUwasilisha maudhui na mawasiliano na wasikilizaji wa Igbo na Yoruba katika lugha mama yao ni jambo la kusisimua na kufurahisha," anasema.

"Tumekuwa na BBC Hausa [lugha inayozungumzwa kaskazini mwa Nigeria] kwa miongo kadhaa na tumeiona athari iliyoleta kwa wasikilizaji.

"Tunapoiangalia Nigeria tuna jamii yenye tamaduni nyingi na BBC ilihisi kwamba ni muhimu kupatia tamaduni zote fursa ya kuwasiliana na kuwa na mazungumzo."

Image caption Lugha zinazotarajiwa kutangazwa katika BBC

Mada zinazohusiana

Kuhusu BBC