Saratani ya Ovari : Kuvimbiwa mara kwa mara inaweza kuwa dalili

Laura Everley na mwanae wa kiume Haki miliki ya picha Laura Everley
Image caption Laura Everley,ambaye alipatikana na saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi(ovari) mwaka 2014, akiwa pamoja na mwanae wa kiume Harry

Ni theluthi moja tu ya wanawake wanaomuona daktari licha ya kuwa na dalili kubwa, wasema utafiti shirika la kupambana saratani ya Ovari-Target Ovarian Cancer.

Unapokabiliwa na kuvimbiwa, 34% ya wanawake 1,142 waliohojiwa na kampuni ya YouGov ndio waliosema wanaweza kumuona daktari.

Nusu walisema hatua ambayo wanaichukua ni kubadili lishe yao kwa kufanya vitu kama kula vyakula vyenye chachu kama maziwa ya mgando ama Yogati

Shirika hilo la kupambana na saratani ya Ovari linafofia kile linachosema ni "viwango vidogo vya uelewa " wa kuvimbiwa kama dalili ya saratani.

Utafiti wa awali uliofanywa na shirika hilo ulionyesha kuwa ni mwanamke mmoja tu kati ya watano anayeweza kung'amua kuwa kuvimbiwa ni dalili ya saratani.

Utafiti huu unazungumzia kuhusu wanawake wote wa Uingereza na waliulizwa ni nini wangekifanya iwapo ''wangekua na tatizo la kuvimbiwa kwa mara kwa mara'' s

Wengi hawakuweza kusema kuwa wanaweza kumuona daktari kutokana na tatizo hilo.

'Huwezi kudhani inaweza kutokea kwako'

Laura Everley, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 38, kutoka eneo la Crawley, alipatikana na saratani ya Ovari mwaka 2014.

Kabla ya kupatikana na ugonjwa huo alisema kuwa alikua amekwishapata dalili zote za saratani ya Ovari ,ikiwemo kuvimbiwa tumbo.

"Nilifikiri labda ni usumbufu tu wa kawaida wa njia ya choo kwasababu dalili zote zinafanana.

" Nilikua hata wakati mwingine nacheua , lakini haikuleta mabadiliko yoyote. Wazo la saratani kwakweli halikuniingia kichwani. Huwezi kuota kwamba inaweza kutokea kwako''.

Kwa sasa amekamilisha matibabu na anaendelea vema.

Haki miliki ya picha Laura Everley
Image caption Laura Everley,ambaye alipatikana na saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi(ovari) mwaka 2014, akiwa pamoja na mwanae wa kiume Harry

Wataalam wa afya wanashauri mtu yeyote mwenye ambaye amekuwa akihisi mwenye kuvimbiwa mara kwa mara kwa kipindi cha wiki tatu kumuarifu daktari wake .

Kuvimbiwa kunaweza kusababishwa nahali nyingine mfano ugonjwa wa njia ya choo, ni dalili pia inayojitokeza kabla ya hedhi, lakini kama hali hii inadumu kwa muda mrefu pila kuisha unahitaji kuangaliwa na daktari.

Ugonjwa huu zaidi unaweza kuwapata wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 55, lakini shirika la kukabilian na saratani ya Ovari nchini Uingereza linasema ni wachache wanaoweza kutambua kuwa inaweza kuwa ni dalili ya saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi.