Thailand: Mwanaume aliyezalisha wanawake tofauti apewa idhini ya kuwalea

Watoto wachanga tisa walipatikana kwenye jengo moja la ghorofa mjini Bangkok Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watoto wachanga tisa walipatikana kwenye jengo moja la ghorofa mjini Bangkok mwaka 2014

Mahakama moja mjini Bangkok,Tailand imemkabidhi raia mmoja wa Japan,idhini ya kuwalea watoto 13, ambao, alizaa na wanawake kadhaa walezi nchini humo.

Nendeni ulimwenguni mukaijaze dunia hivyo ndivyo bwana Mitsutoki Shigeta alivyoiambia mahakama .

Bwana huyo ambaye amekuwa akichunguzwa na shirika la polisi la kimataiafa la Interpol tangu mwaka 2014 aliambia mahakama kwamba sababu za yeye kujihusisha kwa kutoa mbuge zake za kiume kwa wanawake kadhaa lengo lake kubwa lilikuwa ni kuwa na watoto wengi iwezekanavyo.

Wakati polisi hao wa kimataiafa walipovamia jumba lake huko mjini Bangkok palipatikana watoto tisa aliwawazaa kutokana na yeye kutoa mchango wakw wa megu za kiume.

Wakati huo alidhaniwa anafanya biashara ya ulanguzi wa watoto .

Lakini uchungzi wa vinasaba vya DNA vilipofanywa watoto hao wote japo walikuwa wa rangi na sura tofauti walithitishwa ni uzao wake bwana Shigeta

Kong Suriyamontol ni wakili wake , " Jambo lililoamuliwa ni kawmba mteja wangu hahusiki na biashara ya ulanguzi wa binadamu na hana hatia yeyote . Yeye haiba yake ni nzuri na ana njia njema kuasi watoto. Na huu ndio uamuzi wa mahakama hii leo"

Wakili huyo aliwaambia wanahabari kwamba atafanya bidi ili mteja wake apewe watoto wote aliochangia mbegu za kiume.

Lakini wakili mmoja wa uingereza ambaye anashughulika na sheria ya ubebaji mimba kutoka na mbegu ya kiume au ya kike iliyotungishwa kisayansi anasema kuna haja ya kuwepo kwa sheria inayokubalika kimatioafa kulinda watu wanaotaka kutoa mchango wa mbegu ya kiume au hata ya kike kwa wale wasio na uwezo wa kizaa na hata kubeba mimba

Bi Natalie Gamble anaelezea ni kwanini, "Huwezi kabisa kuona mambo kama haya yakifanyika Marekani au Uingereza kwa sababu kuna mikakati ya kisheria na mifumo muafaka.

Kliniki za utungaji mimba ,na mashirika pamoja na mawakili huhakikisha kwamba hakuna dosari inayotokea. Ni wazi kwamba ni muhimu maslahi ya mtoto anayezaliwa kuzingatiwa na kulindwa".

Lakini wakili huyo ameshauri kwamba yeyote anayeingia katika mkataba kama huyo wa kujihusisha kwa kubeba mimba au kuazima mbegu za kiume lazima ahakikishe haki yake inalindwa kisheria

"Changamoto wanaosafiri nchi za nje ni kuhakikisha kwamba kule wanakokwenda sheria ya ubebaji wa mimba inatambuliwa na kuafikiwa wakati wanafanya makubaliono ili kuhakikisha wale wote wanaokubaliana wanakaguliwa vilivyo, kusharuriwa na wanafanya hivyo kwa hiari yao wenyewe, Na endapo mtu atasafiri katika nchi ambapo sheria hizo hazipo , hapo ndipo kuna changamto. Kuna wasiwasi kwamba yule anayeinga katika mkataba wa kubeba mimba hafanyi hivyo kwa hiari yake, akiwa na ufahamu kamili na pia kuna hatari kwamba wewe kama mzazi sheria hizo huenda zikakugeuka katika harakati za ubebaji na utunzi wa mimba ".

Kwa bwana Shigeta badala ya kuijaza dunia kwa njia ya tendo la ngono aliona njia ya mkato ya kuwa na watoto chungu nzima wa kwake mwenyewe ni kutoa mcahngo wa mbegu yake. Sasa ana watoto 13 kutoka mama tofauti tofaut na wa kila rangi.

Mada zinazohusiana