Baba wa mtoto aliyesafirishwa kwenda Uhispania kwa sanduku aepuka kifungo jela

An x-ray shows an eight-year-old boy hidden in a suitcase Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakati maafisa waliikagua sanduku hiyo waliona picha ya mtoto ambaye alikuwa amejikunja

Mwanamume raia wa Ivory Coast, ambaye mtoto wake wa miaka minane alisafirishwa kiharamu kwenda nchini Uhispania kutoka Morocco akiwa ndani ya sanduku ameepuka kifungo jela.

Wakuu wa mashtaka walikuwa wanataka Ali Ouattara kufungwa kwa kuchangia mtoto wake kuingia Uhispania kinyume na sheria.

Hata hivyo hilo liligeuzwa kuwa faini ndogo wakati walisema kuwa hawajapata ushahidi kuwa alifahamu kwamba mtoto wake angesafishwa kwa kutumia sanduku.

"Babangu wala mimi hatukufahamu ikiwa wangeniweka ndani ya sanduku," kijana huyo Adou ambaye sasa ana umri wa miaka 10 aliwaambia majaji.

Adou alisema kuwa Bw Ouattara ambaye alikaa gerezani mwezi mmoja alikuwa amemuambia kuwa safari ingekuwa ya kutumia gari.

Adou alisema alikumbwa na tatizo la kupumua akiwa ndani yab sanduku ambayo ilitumiwa kumvusha kwenye mpaka kati ya Morroco na himaya ya Uhispania ya Cueta.

Image caption Ceuta

Mwezi Mei mwaka 2005 maafisa wa kivuko cha mpaka kati ya Morocco na Ceuta walimsimamisha mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifuruta sanduku nzito.

Wakati waliikagua sanduku hiyo waliona picha ya mtoto ambaye alikuwa amejikunja

Bw Ouattara aliamrishwa kulipa faini ya dola 114.

'Niliuzwa kama mtumwa mara tatu Chad na Libya'

Mtoto sasa anaishi na mama yake mjini Paris lakini alisafiri kwenda Ceuta kutoa ushahidi.

Bw Ouattara anasema familia yake, yeye, mke wake, binti yake na mwanawe huyo wataanza maisha mapya kaskazini mwa Uhispania.

Mada zinazohusiana