Mataifa hatari zaidi kwa watoto kuzaliwa duniani

Kati ya nchi 10 hatari zaidi, 8 kati yazo ziko kusini mwa jangwa la sahara Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kati ya nchi 10 hatari zaidi, 8 kati yazo ziko kusini mwa jangwa la sahara

Watoto wanaozaliwa kwenye nchi maskini zaidi duniani wako kwenye hatari ya kufa mara 50 zaidi ikilinganishwa na wale wanaozaliwa kwenye nchi tajiri, kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Licha ya kuboreska kwa afya kwa watoto wa umri mkubwa robo la mwisho ya karne iliyopita, "hatujapata mafaniko katika kuzuia vifo miongoni mwa watoto walio na chini mwezi mmoja," alisema Henrietta Fore mkurugenzi wa UNICEF.

Tofauti ni kubwa. Mtoto anayezaliwa nchini Pakistan ambayo ni nchi yenye viwango vya juu zaidi vya vifo vyaa watoto, kuna kifo cha mtoto mmoja kati ya watoto 22, huku mtoto mmoja ndiye anaweza kufariki Japan kati ya 1,111 kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Zaidi ya asilimia 80 ya vifo vya watoto wanaozaliwa vinaweza kuzuiwa ikiwa kutakuwa na wakunga wenye ujuzi, huduma kama za maji safi, madawa, unyonyeshaji saa ya kwanza baada ya mtoto kuzaliwa na lishe bora.

Kati ya nchi 10 hatari zaidi, 8 kati yazo ziko kusini mwa jangwa la sahara ambapo wanawake wajawazito wana uwezo wa chini kupata msaada kutokana na umaskini, mizozo na mifumo duni, kulingana na ripoti.

Nchi hizi ni Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyo na mtoto mmoja kati ya 24, Somalia, Lesotho, Guinea-Bissau na Sudan Kusini kifo kimoja kati ya 26, Cote d'Ivoire kifo kimoja kati ya 27 na Mali na Chad zote zikiwa na kifo kimoja kati ya 28.

Kila mwaka watoto milioni 2.6 hawaishi mwezi wao wa kwanza wa kuzaliwa.

Vifo vinaweza kuzuiwa

Ripoti hiyo ilitolewa wakati wa kuzinduliwa kwa kampeni ya dunia nzima yenye kauli mbiu Kila Mtoto Aishi, yenye lengo la kuhakikisha kuwepo kwa huduma za afya nafuu kwa kila mama na mtoto anayezaliwa.

Zaidi ya asilimia 80 ya vifo vya watoto wanaozaliwa vinaweza kuzuiwa, ripoti hiyo ilisema, ikiwa kutakuwa na wakunga wenye ujuzi, huduma kama za maji safi, madawa, unyonyeshaji saa ya kwanza baada ya mtoto kuzaliwa na lishe bora.

Image caption Zaidi ya asilimia 80 ya vifo vya watoto wanaozaliwa vinaweza kuzuiwa

Ukosefu wa wahudumu wa afya wenye mafunzo yanayostahili na wakunga ndio nchangamoto kubwa kwenye nchi maskini.

Wakati nchi tajiri kama Norway ina madakati 18, wauguzi na wakunga kwa kila watu 10,000, nchi maskini kama Somalia zina daktari mmoja tu. Kila mwaka watoto milioni moja hufariki ile siku wanazaliwa.

Nchi zinaweza kufanikiwa kwa njia gani

Kwa jumla watoto wal;iozaliwa kwenye nchi tajiri wana nafasi nzuri lakini kuna tofauti kati ya nchi. Watoto wanaozaliwa kwenye familia maskini wako asilimia 40 zaidi ya kufa wakilinganishwa na wale wanaozaliwa kwenye familia ambazo si maskini.

Kwa mfano hii ni hadithi ya Mary James mwanamke wa umri wa miaka 18 kutoka kijiji kimoja nchini Malawi. Wakati uchungu wa kuzaa ulianza, yeye na dada yake walianza safari ndefu ya kutembea kwenda kwa kituo cha afya.

Wakati mtoto alizaliwa, alikuwa mdogo na mnyonge sana.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watoto wanaozaliwa kwenye familia maskini wako asilimia 40 zaidi ya kufa wakilinganishwa na wale wanaozaliwa kwenye familia ambazo si maskini

Anasema wahudumu walifanya kila wawezalo lakini ilipofika usiku mtoto akafa. "Nilihisi kuwa moyo wangu ungepasuka," James aliwaambia wafanyakazi wa UNICEF. "Nilikuwa na jina la mtoto lakini hakufungua macho yake."

Kwa sababu kuboresha huduma za afya yaweza kuwa ghali , "ni muhimu kuwekeza pesa hizo kwa njia inayofaa," mkuu wa mpanngo wa uzazi wa shirika la UNICEF Willibald Zeck aliiambia AFP.

Hii inaweza kumaanisha kuwa kitu kama kuhakikisha mwanamke mjamzito ambaye ametembea kwa siku tatu kwenda kwa kituo cha afya amepokelewa kwa heshima ili kubaki kwa muda na kutunzwa kwa muda baada ya kujifungua.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Nchi zenye viwango vya chini zaidi kwa vifo vya watoto baada ya Japan ni zile nchi zenye mifumo mizuri ya elimu na afya

Kati ya nchi ambazo zimefanikiwa sana ni Rwanda ambayo imepunguza kwa nusu kutoka mwaka 1990 hadi mwaka 2016 na kuonyesha umuhimu wa siasa katika kuwekeza katika mifumo mizuri ya afya, ripoti hiyo ilisema.

Nchi zenye viwango vya chini zaidi kwa vifo vya watoto baada ya Japan ni zile nchi zenye mifumo mizuri ya elimu na afya zikiwemo: Iceland kifo kimoja katika ya 1,000, Singapore (kifo kimoja kati ya 909), Finland (kifo kimoja kati ya 833), Estonia na Slovenia (zote kifo kimoja kati ya 769), Cyprus (kifo kimoja kati ya 714) na Belarus, Luxembourg, Norway na Korea Kusini (zote kifo kimoja kati ya 667).

Mada zinazohusiana