Wakimbizi wa DRC nchini Rwanda waapa kurudi nyumbani baada ya kupunguziwa mlo

Wakimbizi wa Kongo wakiwa kambini nchini Rwanda

Wakimbizi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliotoka katika kambi ya Kiziba magharibi mwa Rwanda kwa siku ya pili wameendelea kukita kambi katika ofisi za shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi katika mji huo wa magharibi wakishinikiza kurudishwa kwao au kutafutiwa nchi ya tatu.

Shirika hilo limewambia kuwa swala hilo limeliweka mikononi mwa serikali ya Rwanda jambo ambalo wakimbizi wamesema hawataki hata kusikia.

Rwanda imewataka kurudi katika kambi yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa.

Tangu asubuhi sehemu waliko kumezingirwana vikosi vya jeshi la polisi.

Awali wakimbizi hao , walisema kuwa wanajeshi wa Rwanda waliwapiga risasi na kuwajeruhi wawili miongoni mwao.

Wanadai walipigwa risasi Jumanne walipokua wakijaribu kutoka nje ya kambi kwa maandamano ya kupinga kukatwa kwa mgao wa chakula.

Serikali ya Rwanda imekanusha madai hayo. Waziri wa masuala ya wakimbizi na udhibiti wa majanga De Bonheur Jeanne d'Arc amesema ''"Bado tunajadiliana juu ya kile kinachopaswa kufanyika, lakini tunadhani hakuna mkimbizi anayepaswa kujaribu kurejea nyumbani Congo kama njia ya mgomo''

"askari hawakumpiga risasi yeyote. Askari waliwazuwia kutoka kambini na wakimbizi wakaanza kurusha mawe

Kwa vyovyote vile watu wanapoanza kurusha mawe wakiwa wengi kama walivyokua, baadhi yao wanajeruhiwa.

Image caption Askari wa Rwanda wakiwa tayari kuwakabili wakimbizi

''Sina taarifa zozote kwamba walipiga risasi hata moja hewani'' Alisisitiza waziri De Bonheur Jeanne d'Arc. Wakimbizi wapatao 2,000 kutoka kambi ya yenye wakimbizi 17,000 iliyopo eneo la Karongi kusini mwa Rwanda walitoka nje ya kambi yao kupinga kukatwa kwa asilimia 25 ya mgao wa chakula wanachopewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la huduma kwa wakimbizi (UNHCR) tangu mwezi uliopita.

Shirika hilo linasema lilikata msaada huo kutokana na matatizo ya kifedha yanayolikabili

" Tulipofika katika mji wa Karongi askari walitusimamisha, askari mmoja aliekua na gari akawaambia wengine wafyatuer risasi ," Alisema Eugene.

Mukabasoni, mama wa watoto watatu alipozungumza na shirika la habari la Reuters by kwa njia ya simu na kuongeza kuwa askari waliwapiga vibaya wakimbizi.

" Nilipigwa kichwani na fimbo," alisema Eugene. Wakimbizi wengine waliozungumza na waandishi mwandishi wa BBC wa Kigali walitoa madai kama hayo, baadhi yao wakimuonyesha majeraha ya kupigwa.

Rwanda imewapokea wakimbizi wapatao 174,000 , wakiwemo 57,000 waliotoka taifa jirani la Burundi.

Kiongozi wa wakimbizi wa DRC, Louis Maombi, ameapa kuwa hawataondoka hadi suala lao litakapotatuliwa. Kambi ya Kizibaina jumla ya wakimbizi 17,000 waliokimbia mapigano nchini Kongo mwaka 1996.

Maafisa kutoka shirika la UNHCR hawakuweza kutoa kauli yoyote kuhusiana na kisa hicho. Hata hivyo inatarajiwa kwamba shirika hilo na serikali wataitisha kikao na waandishi wa habari leo Jumatano kuzungumzia tukio hilo.

Mada zinazohusiana