Wakristo wa Colombia wenye asili ya Afrika wanaosherehekea Krismasi Februari

Wakazi wa kijiji cha Colombia cha QuinamayĆ³ wamekuwa wakisherehekea Krismasimwezi huu wakiwa na sanamu ya mtoto Yesu mweusi.

Wakolombia wenye asili ya Afrika wakiwa wameshikilia kikapu chenye sanamu ya "Nino Dios" (Mungu mwana) ndani katika kijiji cha Quinamayo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kati sherehe hizi kuna sanamu ya mbao ya mtoto Yesu

Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo.

Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo.

Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia.

"Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe.

Msichana wa Colombia mwenye asili ya Afrika akishiriki katika sherehe za kuabudu sanamu maarufu kama "Adoraciones al Nino Dios" katika kijiji cha Quinamayo, kitengo cha of Valle del Cauca nchini , Colombia, Februri 18, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanakijiji wanasema kizazi kichanga kimekuwa muhimu katika kuutunza utamaduni huo

"Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hivyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw Larrahondo.

Balmores Viafara, mwalimu mwenye umri wa miaka 53 aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kutokana na hilo kwake tarehe 24 Disemba "ni kama siku nyingine yoyote ile ".

Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu."

Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu", ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.

Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi.

Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo.

Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.

Watoto wa Kolombia wenye asili ya Kiafrika wakiwa waliovalia mavazi rasmi wakishiriki katika sherehe za ibada ya "Adoraciones al Nino Dios" katika kijiji cha Quinamayo, nchini Colombia tarehe 18 Februari, 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Utamaduni huu ulianza tangu enzi za utumwa
Densi ya kitamaduni ya "Fuga" ya waColombia wenye asili ya Afrika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa densi ya "Fuga" wakidensi kwa kuigiza watumwa waliofungwa minyororo
Mwanamume mmoja akirekodi picha za fataki kwa simu yake ya mkononi katika sherehe za "Adoraciones al Nino Dios" katika kijiji cha Quinamayo, kilichopo kwenye idara ya Valle del Cauca, nchini Colombia, Februari 18, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufyatuaji wa fataki huchukua sehemu kubwa ya sherehe

Picha zote haziruhusiwi kunakiliwa bila idhini ya mwenye haki miliki

Mada zinazohusiana