Majambazi wavamia kituo cha polisi na kuwaua polisi 5 Afrika Kusini

Police officers Haki miliki ya picha AFP
Image caption The attackers took 10 firearms and a police van from the station

Polisi watano na mwanajeshi mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa uvamizi kwenye kituo cha polisi kwenye mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika kusini.

Katika taarifa serikali ya shirika la habari la serikali nchini Afrika Kusini ni kuwa polisi watatu waliuawa papo hapo.

Mwanajeshi ambaye hakuwa kazini alipigwa risasi na majambazi hao wakati wakati wakitoroka wakiwa pia nwameshika mateka polisi wawili. Miili yao ilipatikana umbali wa kilomita sita.

Kundi hilo la majambazi waliokuwa wamejihami walivamia kituo cha polisi karibu na Umatata na kufyatua risasi mapema leo.

Polisi bado hawajui kiini cha shambulizi hilo. Washukiwa wanaaminiwa kupora mashine ya kutoa pesa muda mfupi kabla ya kuvamia kituo cha polisi. Walichukua bunduki 10 na gari la polisai kutoka kituo hicho.

Gen Khehla John Sitole, kamishna wa idara ya polisi nchini Afrika Kusini ameapa kuwapata wauaji hao.

Mada zinazohusiana