Mambo sita ambayo aliyaamini Billy Graham

American evangelist Dr Billy Graham addressing the congregation at Earl's Court - June 1966 Haki miliki ya picha Fox Photos/Getty Images
Image caption Graham akizungumza huko Earl's Court mjini London mwaka 1966

Mwinjilisti mmarekani Billy Graham, mmoja wa wahubiri maarufu zaidi katika karne iliyopita amefariki akiwa na miaka 99.

Katika taaluma yake ambayo ilidumu zaidi ya miaka 60, anaaminiwa kuwahubiria mamilioni ya watu kwenye mikkutano yake.

Haya ni baadhi ya masuala aliyoyaamini na kusimama nayo kwenye maisha yake.

1. Alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu mapema.

Wakati wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani, Graham alisema kuwa hangeweza kuhubiria watu waliogawanyika miaka ya 1950 na pia alizungzia suala la kujumuika.

Katika warsha moja huko Tennessee mwaka 1953 aliondoa kamba zilizotenganisha wazungu na watu weusi kwa wale aliokuwa akiwahubiria.

"Ukiristo sio wa watu weupe na usiruhusu mtu akuambie ni wa watu weupe au weusi," aliambia umati nchini Afrika Kusini mwaka 1973.

Graham pia alikuwa rafiki wa karibu wa Martin Luther King Jr, na wakati mmoja alimlipia dhamana alipokamatwa wakati wa maandamano mwaka 1960.

2. Ilikuwa muhimu kuwafikia wale usiowajua

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Graham (katikati) akikutana Kim Il-sung nchini Korea Kaskazini mwak 1992

Mwaka 1992 Graham alikuwa mwinjilisti wa kwanza wa kigeni kuzuru taifa la Korea Kaskazini ambapo alikutana na kiongozi wake Kim Il-sung. Pia alirudi miaka miwili baadaye.

Familia yake ian uhusiano wa karibu na Korea Kaskazini-aliyekuwa mke wa Graham marehemu Ruth, ambaye wazazi wake walikuwa ni wamishenari, alikulia huko Pyongyang miaka 1930.

Katika ziara hiyo ambapo Graham alizungumza kuhusu imani yake mbele ya watu wa chuo kikuu, ilifanyika baada ya idhini ya Rais George HW Bush.

Ziara hiyo ilisababisha Graham kutajwa na wengine kama mjumbe asiye rasmi wa Marekani kwenda nchi ambazo hazikuwa na uhusiano mzuri na Marekani wakat huo. Mwaka 1984 alifanya ziara ya siku 12 katika Muungano wa Usovieti na hata kukutana na maafsa wa muugano huo.

3. Sheria ya Billy Graham

Ikiwa pia inajulikana kama sheria ya Mike Pence.

Sheria hiyo kuhusu kuzuia hisia zote kwa mwanamke ilibuniwa na Graham na wainjilisti wengine watatu mwaka 1948 na inahusu ushauri wa Paulo wa Timoteo kwenye Biblia.

Hadi sasa inatumiwa na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence.

"Tulijiahidi na kuzuia hali yoyote ambayo ambayo ni ya kutiliwa shaka, Graham alisema. "Kutoka siku hiyo, sikusafiri, kukutana au kula peke yangu na mwanamke mwingine asiye mke wangu."

4. Kuna matumaini hata wakati wa nyakati ngumu zaidi

Akizungumza huko Washington siku tatu baada ya shambulizi la Septemba 11 mwaka 2001, Graham alisema kuwa alikuwa na wakati mgumu kupata majibu.

"Nimeulizwa mara mia kadhaa ni kwa nini Mungu aliruhusu taabu kama hii. Ningepeda kusema kuwa sina jibu," alisema, akiongeza kuwa janga hilo lilikuwa ni funzo kwetu kuhusu kumjali mwingine.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Billy Graham akihubiri huko Trafalgar Square mjini London

5. Kila mtu lazima aokolewe hata mhalifu mbaya

Moja ya masuala yanayokumbukwa katika maisha yake Graham ni wakati alifanya urafiki na mkuu wa genge la wahalifu la Los Angeles Mickey Cohen.

Hata hivyo Cohen hakuitia ombi la Graham la kumtaka aokoke lakini aliendelea na urafiki huo kwa miaka mingi akisema mhalifu anaweza kuwa mhubiri ikiwa angechagua kufanya hivyo.

Cohen hakuitikia wito huo wa Graham.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Billy Graham akiwa Paris mwaka 1986

6. Alijutia kujihusisha na masuala ya siasa

Kwa miongo kadhaa Graham alihusika na masuala ya White House na kuhudumu kama mshauri asiye rasmi kwa marais.

Aliishia kuwa rafiki wa karibu wa marais hasa Lyndon Johnson na Richard Nixon.

Urafiki wa Graham na Nixon ulikuwa mkubwa hata kuishia kumshuri rais kuhusu ni hatua gani angechukua nchini Vietnam

Mwaka 2011 wakati wa mahojiano na Christianity Toda, Grahama alisema anajutia kujihusisha na masuala ya siasa