Nyota Lupita Nyong'o kushiriki kwenye filamu ya mcheshi Trevor Noah

Nyota Lupita Nyong'o na Mchekeshaji Trevor Noah Haki miliki ya picha Instagram/LupitaNyong'o
Image caption Nyota Lupita Nyong'o na Mchekeshaji Trevor Noah

Nyota wa tuzo ya Academy Lupita Nyong'o anatarajia kushiriki katika filamu itakayo tengenezwa kutoka kwa kitabu cha 'Born a Crime' ambacho ni simulizi ya maisha ya mchekeshaji, raia wa Afrika Kusini Trevor Noah.

"Sikuweza kukiweka kitabu chini. Ninafuraha kutangaza kwamba nitahusika na kutayarisha filamu juu ya kitabu hicho!" Nyong'o alisema katika Ukurasa wake wa Instagram.

Noah ni mtangazaji wa mojawapo ya vipindi vya runinga vyenye shinikizo kubwa Marekani, The Daily Show, alijibu kwa kusema katika ukurasa wake wa Twitter "Niko mbinguni"

Alielezea zaidi kwenye ukurasa wake wa Instagram, akisema Nyong'o -aliyekuwa mhusika katika filamu yenye mafinikio kubwa hivi karibuni ya Black Panther - "anafaa sana" kuigiza kama mama yake Noah.

"Mama yangu ni mwanamke shupavu ambaye ni rahisi sana kumuona kama mmoja ya mashujaa wa Wakanda. Kwa hiyo inafaa sana kwa mama yangu kuigwa na mrembo kama Lupita Nyong'o. Nimefurahi sana." aliandika

Kitabu cha 'Born a Crime' ni simulizi ya Noah akikulia katika enzi za ubaguzi Afrika Kusini kama mtoto wa mwanamke mweusi na baba mzungu.

Mada zinazohusiana