Saudi Arabia yatangaza dola bilioni 64 kwa burudani

Cinema is seen with red carpet and Captain Underpants banners hanging

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mkuu wa halmashauri ya burudani anasema kuwa warsha 5,000 zimepangwa mwaka huu pekee zikiwemo zile za Maroon 5 na Cirque du Soleil.

Saudi Arabia inasema kuwa itawekeza dola bilioni 64 katika kuijenga sektaa yake ya burudani katika kipindi cha miaka 10 inayokuja.

Mkuu wa halmashauri ya burudani anasema kuwa warsha 5,000 zimepangwa mwaka huu pekee zikiwemo zile za Maroon 5 na Cirque du Soleil.

Ujenzi wa ukumbi wa kwanza nchini humo umeanza mjini Riyadh.

Uwekezaji huu ni sehemu ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yanayofahamika kama Maono ya mwaka 2030 yaliyozinduliwa miaka miwili iliyopita na mrithi wa ufalme Prince Mohammed bin Salman.

Mrithi huyo wa ufalae mwenye miaka 32 anataka kuboresha uchumi na kuzuia taifa hilo kutegemea mafuta .

Mwezi Disemba serikali iliondoa marufuku ya sinema za biashara.

Mkuu wa halmashauri ya burudani Ahmed bin Aqeel al-Khatib alinukuliwa na vyombo vya habari akisema anatarajia kuwa watu 220,000 wataajiriwa katika sekta ya burudani ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 kutoka watu 17,000 mwaka uliopita.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwezi Januari, kundi Cirque Eloize lilizuru Saudi Arabia kwa mara ya kwanza

Mji mkubwa wa burudani karibu na mji wa Riyadh, karibu ukubwa na mji wa Las Vegas, tayari umepangwa kujengwa wakati nchi inalenga kuboresha sekta yake ya uchumi.

Hii ni baada ya mabadiliko mengine ambayo yameshuhudiwa katika taifa hilo ikiwemo kuruhusu wanawake mashabiki wa kandanda kuhudhuria mechi za kandanda mwezi uliopita na kutangaza kuwa wanawake wataruhusiwa kuundesha magari.

Mwaka uliopita Prince Mohammed alitangaza kwa lengo lake ni kwamba Saudi Arabia itakuwa nchi ya itakaribisha dini zote, tamaduni na watu.