Mwili wa Akwelina waagwa

Picha ya Akwelina Akwilini ilipambwa na maua katika ibada ya kuaga mwili wake
Image caption Picha ya Akwelina Akwilini ilipambwa na maua katika ibada ya kuaga mwili wake

Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi juma lililopita Akwelina Akwilini umeagwa na kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi siku ya Ijumaa wiki hii.

Katika ibada ya heshima za mwisho ilyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT hapo Padri Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohane Mbatizaji Luhanga, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka mtu aliyempiga risasi mwanafunzi huyo Akwelina Akwilini, na kumuweka wazi ili awaombe radhi Watanzania.

Image caption .

Akwelina Akwilini alipigwa risasi na Polisi juma lilopita siku ya Ijumaaa wakati kikosi cha polisi kitengo cha kutiliza ghasia,FFU, kilipokuwa kikiwakabili waaandamanaji wa chama cha upinzani cha CHADEMA baada ya kumaliza Kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni,jijini Dar es salaam.

Katika ibada hiyo pia liliibuka kundi la wanafunzi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakitaka haki itendeke, mabango ambayo waliyainua punde Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako alipo anza kuzungumza. Lakini pingamizi lao likasitishwa na askari awalio chukua mabango hayo na kuyachana.

Image caption Makamu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika(wa pili kutoka kulia) ni baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hio

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa asasi za kiraia, wanaharkati wa haki za binadamu na chama cha taifa cha wanafunzi za kumtaka Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba.

Hadi sasa polisi wamwatia mbaroni polisi 6 wanaodaiwa kuhusika katika kuuwawa kwa manafunzi huyo.

Image caption Mamia ya Watanzania wajitokeza kwenye viwanja vya Chuo cha usafirishaji Tanzania NIT kuaga mwili wa mwanafunzi

Maadhimisho Haya ya ibada misa takatifu yamehudgiriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali wakimwo Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndaluchako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Enjinia Hamad Masauni.

Mada zinazohusiana