Afrika kwa Picha Wiki Hii (16-22 Februari 2018): Tembo wanafanya nini angani?

Mkusanyiko wa picha bora kutoka Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii:

Kenya Wildlife Service lift a tranquillized elephant bull into an truck at the Lamuria, Nyeri county, on February 21, 2018 during the transfer of elephants from Solio, Sangare and Lewa to northern part of Tsavo East National Park in Ithumba.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Si kawaida kuwaona ndovu wakiwa angani - lakini Jumatano wiki hii katika kaunti ya Nyeri, Kenya hiki ndicho kilichotokea. Tembo hawa walikuwa wanahamishwa kutoka hifadhi za Solio, Sangare na Lewa hadi maeneo ya kaskazini ya mbuga ya taifa ya Tsavo Mashariki eneo la Ithumba.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mjini Abidjan, Ivory Coast binadamu ndio waliokuwa wanapaa katika tamasha ya kwanza ya aina yake ya maonesho ya sarakasi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nchini Zimbabwe mamia walikusanyika kumuomboleza kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai, aliyefariki dunia akiwa na miaka 65.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Siku hiyo pia, mama alikuwa amejaliwa mtoto katika hospitali moja Juba, Sudan Kusini. Taifa hilo ni miongoni mwa maeneo hatari zaidi duniani kwa mtoto kuzaliwa, kwa mujibu wa ripoti ya Unicef iliyotolewa wiki hii.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nchini Ethiopia, wahanga walikumbuka Mauaji ya Addis Ababa ambapo zaidi ya raia 20,000 wa Ethiopia waliuawa na wanajeshi wa Italia mnamo 19 Februari, 1937.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Libya raia walikuwa pia wanaikumbuka tarehe muhimu wiki hii. Mnamo 17 Februari yalipoanza maandamano ambayo mwishowe yalichangia kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Nchi jirani ya Misri maandalizi ya uchaguzi yaliendelea. Wafuasi wa rais wa sasa wanaonekana wakiweka bango mjini Cairo mnamo 21 Februari.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Afrika Kusini nako kulikuwa na rais mpya, lakini hakuingia madarakani kupitia uchaguzi. Cyril Ramaphosa hapa anaonekana wakati wa kutoa hotuba kwa kataifa. Mwanamke huyu alimuona?

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Upande mwingine wa dunia nchini Korea Kusini, mchezaji wa Ghana wa kuteleza kwenye barafu Akwasi Frimpong alimtambulisha binti yake kwa rafiki wakati wa mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi PyeongChang.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Lakini Kenya, macho yalikuwa yanaangazia mashindano mengine makubwa yajayo - Michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Australia Aprili. Hapa, washiriki wa mbio za mita 800 wanashindana wakati wa mchujo wa kuchagua watakaowakilisha taifa hilo uwanjani Kasarani, Nairobi mnamo 17 Februari.

Picha kwa hisani ya AFP na EPA