'Ufyozi' wa Kylie Jenner waangusha hisa za Snap Chat na kuugharimu mtandao huo $1.3bn

Kylie Jenner ni dada wa kambo wa nyota wa Reality TV Kim Kardashian
Image caption Dada wa kambo wa nyota wa Reality TV Kim Kardashian

Nyota wa Reality TV Kylie Jenner aliugharimu mtandao wa Snap Chat thamani ya $1.3bn (£1bn) baada ya kutuma ujumbe wa Twitter kwamba hautumii tena mtandao huo.

Dada huyo wa kambo wa Kim Kardashian alichapisha ujumbe uliosema: Je kuna mtu mwengine ambaye hatumii mtandao wa snap chat ama ni mimi pekee..mh haya ni makosa.

Hisa za mtandao huo zilishuka baada ya Snap chat kuwabadilishia programu wafuasi wa nyota huyo wapatao milioni 24.5.

Wafuasi milioni moja wa mtandao huo waliwasilisha ombi katika mitandao ya kijamii wakitaka Snap kutobadilisha programu hiyo.

Baada ya hisa hizo za snapchat kuanguka zillifungwa zikiwa asilimia 6 na sasa zimerudi karibu na bei yake ya $17 zilipoanza kuuzwa wakati kampuni hiyo iliopingia katika soko la hisa.

Snapchat inakabiliwa na ushindani mkali kutoka Instagram inayomilikiwa na facebook hususan miongoni mwa watu maarufu wanaotumia mtandao huo na shambulio hilo la bi Jenner linajiri wakati ambapo wawekezaji wana wasiwasi.

Hatahivyo Bi Jenner baadaye alituma ujumbe wake akisema: 'hatahivyo nakupenda Snap kwa kuwa mpenzi wangu wa kwanza'.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii