Wakimbizi 5 wa DR Congo wafariki katika makabiliano na polisi Rwanda

Gari la Ambulance likiwabebwa waliojeruhiwa baada ya polisi kuwafyatulia risasi wakimbizi waliokuwa wakiandamana
Maelezo ya picha,

Gari la Ambulance likiwabebwa waliojeruhiwa baada ya polisi kuwafyatulia risasi wakimbizi waliokuwa wakiandamana

Polisi inasema watu 5 wameuawa miongoni mwa wakimbizi wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo waliotawanywa jana huku 27 wakijeruhiwa wakiwemo polisi 7 .

Msemaji wa polisi Theos Badege amesema polisi ililazimika kutumia nguvu ili kuvunja kile kilichokuwa kimeonekana kama kambi mpya ya wakimbizi kwenye makao ya shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi na kwamba walizusha ghasia dhidi ya polisi kwa kurushia mawe, vyuma na chupa.

Kulingana na badege tayari wakimbizi 15 wamekamatwa na wanahojiwa na polisi.

Maelezo ya sauti,

Rais Kabila: Hali ni shwari DR Congo

Taarifa kutoka upande wa wakimbizi zinasema kuwa viongozi wao hawajulikani waliko, na inakisiwa kuwa miongoni mwa waliokufa, kutoweka, kuzuiliwa aukuwa ,iongoni mwa waliopelekwa hospitalini

Maelezo ya picha,

Wakimbizi wa DR Congo nchini Rwanda

Wakimbizi hao waliandamana siku 4 zilizopita wakitoka katika kambi yao ya Kiziba hadi shirika la Umoja wa Mataifa kushinikiza warudishwe nchi mwao au watafutiwe nchi ya tatu.

Kambi ya kiziba inahifadhi wakimbizi wapatao elfu 17 waliotoroka Congo miaka 22 iliyopita.

Mmoja ya wakimbizi waliohusika pakubwa kuwasafirisha waathiriwa hopsitali ambaye alizngumza na mwandishiu wa BBC Yve Buchana alisema:

Kwanza wamepiga risasi, tukawambia kwamba hatupambani nao, wakaendelea kupiga risasi watu wakatapakaa kila sehemu, wakaendelea kufyatua risasi na wengine wakaanza kuanguka ,mimi nimeshuhudia watu watatu waliokufa, kuna majeruhi kadhaa tuna wasi wasi kwamba mle ndani kunaweza kuwepo maiti nyingi''

Maelezo ya picha,

Wakimbizi baada ya kutawanywa na maafisa wa polisi. Inakadiriwa kwamba idadi ya wakimbizi waliofariki huenda ikawa ya juu

Kulingana na mwandishi huyo alishuhudia magari ya kubeba wagonjwa ama Ambulance yakipishana na magari ya polisi yakiwa yanabeba majeruhi na watu wengine walioonekana kuwa katika hali mahtuti.

Amesema kwamba upande wa polisi hakuna tamko lolote lililotolewa kufikia sasa licha ya kamanda wa jeshi kanda ya magharibi kumwambia kwamba wakimbizi wamechokoza polisi na kuwarushia mawe.

Tangu jana eneo hilo lilikuwa limezingirwa na vikosi vya polisi waliojihami sawa wakionekana kuwa tayari kwa lolote.Serikali iliiwashutumu wakimbizi kwa kufanya mgomo na kukiuka sheria za nchi na kusema itaanzisha upelelezi kuhusu chanzo cha mgomo huo na kuwaadhibu wahusika.

Wakimbizi wenyewe walisema waliamua kukita kambi kwenye ofisi za shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wakilalamika kuchoka na maisha wanayotaja kuwa mabaya nchini Rwanda huku wakishinikiza kurudishwa nchini mwao au katika nchi nyengine ya tatu.