Nyota wa filamu za Bollywood afariki kutokana na mshutuko wa moyo

Sridevi at a function in Dubai

Chanzo cha picha, Mr Jayakumar

Maelezo ya picha,

Sridevi akiwa Dubai, alipigwa picha hii muda mfupi kabla ya kufariki

Mwigizaji nyota wa Bollywood Sridevi Kapoor amefariki kutokana na mshutuko wa moyo akiwa na miaka 54, familia yake imesema.

Mwigizaji filamu huyo ambaye anafahamika kama Sridevi alikuwa na familia yake mjini Dubai kuhudhuria harusi wa mpwa wake.

Ameshiriki filamu kwa miongo mitano katika filamu 300 kama Mr India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.

Alitajwa kuwa mmoja wa wasanii wachache wa kike waliopata mafanikio makubwa bila ya msaada wa wanaume.

Kutoka akiwa na umri wa miaka minne alikuwa ameshikiri filamu za lugha za Tamil, Telugu, Malayalam, Kannada na Hindi

Umati ulikusanyika nje ya nyumba yake mjini Mumbai wakati habari za kifo chake zilifichuka. Viongozi na wacheza filamu walielezea kushangazwa na kifo chake.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi aliandika katika mtandao wa twitter kuhusunishwa kwake huku naye rais wa India Ram Nath Kovind akisema kifo chake kumewavunja moyo mamilioni ya mashabiki.