Korea Kaskazini wanataka kufanya mazungumzo na Marekani

South Korea's President Moon Jae-in (L), his wife Kim Jung-sook (C), US White House adviser Ivanka Trump (C-R), North Korean General Kim Yong Chol (back R), and United States Forces Korea commander General Vincent K. Brooks (back 2ndL) attend the closing ceremony of the Pyeongchang 2018 Winter Olympic Games at the Pyeongchang Stadium on February 25, 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jenerali wa Korea Kaskazini na Ivanka Trump walishangilia kutoka eneo moja

Korea Kaskazini ina nia ya kufanya mazungumzo na Marekani, kwa mujibu wa Korea Kusini.

Tangazo hilo limekuja baada ya Jenerali Kim Yong-Chol kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kabla ya sherehe za kufungwa kwa mashindano ya olimpiki wa msimu wa baridi.

Binti ya rais wa Marekani Donald Trump Ivanka pia alihudhuria sherehe hizo, lakini maafisa wa Marekani wamekana kufanya mkutano na ujunbe kutoka Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Waandamanaji wa Korea Kusini waliandamana kupinga ziara ya Kim Yong-Chol

Marekani inasema Korea Kaskazini ilijiondoa kutoka kwa mkutano na Makamu wa Rais Mike Pence wakati wa sherehe za ufunguzi.

Eneo la rasi ya Korea limegawanyika tangu vita vya mwaka 1950 hadi 1953 na pande hizi mbili hazijawai weka sahihi mkataba wa amani.

Uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Kusini umeonekama kama njama ya Korea kuvuruga ukaribu kati ya Korea Kusini na Marekani.

Haki miliki ya picha Pool
Image caption Marekani inasema Korea Kaskazini ilijiondoa kutoka kwa mkutano na Makamu wa Rais Mike Pence wakati wa sherehe za ufunguzi

Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.

Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini.

Mada zinazohusiana