Kampuni ya China Greely, yanunua hisa nyingi kwenye Mercedes-Benz

Mercedes Benz' characteristic star

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mercedes-Benz

Kampuni ya kuunda magari ya China Geely, imekuwa mwekezaji mkubwa kwenye kampuni mmiliki wa magari ya Mercedes-Benz, Daimler, ikisema ina matumaini ya kushirikiana na kampuni hiyo kubwa ya Ujerumani katika kuunda magari ya yanayotumia umeme.

Hisa za Geely zilipanda huko Hong Kong baada ya makubaliano ya kununua asilimia 10 ya kampuni ya Daimler kutangazwa wikendi.

Kampuni hiyo ya China tayari inamiliki kampuni yote ya kuunda magari ya Sweden, Volvo.

Mwenyekiti Li Shufu anatarajia kukutana na maaafisa wa Daimler leo Jumatatu na maafisa wa serikali ya ujerumani baadaye wiki hii.

China inaaminika kwa na soko muhimu zaidi duniani kwa makampuni ya kuunda magari.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Magari ya Geely hayana umaarufu mkubwa China

Katika taarifa ya Greely, Bw Li alisema anataka kuandamana na Daimler katika kuwa kanpuni kubwa zaidi kuunda magari wa umeme duniani.

Pia mwishoni mwa wiki, Daimler ilitangaza dola bilioni 1.9 za kuwekeza katika ushirikiano na kampuni nyingine ya magari ya China BAIC.

Pesa hizo zitatumiwa katika kuboresha kiwanda cha BAIC cha kuunda magari ya Mercedes yakiwemo yanayotumia umeme.

Wiki iliyopita kampuni nyinginje ya Ujerumani ya BMW ilitangaza maafikiano na kampuni ya China, Great Wall Motor, kununua magari ya umeme kwa soko la China.