Gesi ya Klorini yatumiwa Syria

Waathiriwa wa mashambulizi Syria

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Waathiriwa wa mashambulizi Syria

Maafisa wa Afya nchini Syria katika maeneo ya waasi yaliyozingirwa kaskazini mwa Ghouta wamesema watu kadhaa wamedhurika kutokana na na dalili zinazoonesha kuathiriwa na gesi ya Klorini, wakati wa mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na majeshi yanayounga mkono serikali.

Taaarifa uiliyotolewa na Wizara ya Afya inayoendeshwa na wapinzani imesema waathirika, madereva wa magari ya kubeba wagonjwa na watu wengine wameripotiwa kuvuta gesi hiyo ya Klorini baada ya mlipuko.

Watu 18 wanatibiwa kwa kuwekewa Oxygen.

Mkazi mmoja katika eneo la mashariki ya Ghouta ameiambia BBC kuna mtoto pia ameathirika.

Dokta Mohammed Khatoub aliyeko Uturuki, ambaye anatokea katika mji wa Ghouta ameelezea uthibitisho wa hospital wanakotibiwa majeruhi hao, kwamba wameathiriwa na gesi hiyo.

Hata hivyo Serikali ya Syria siku zote imekuwa ikikanusha kutumia silaha za kemikali.

Mashambulizi ya ardhini yalipamba moto jana Jumapili, licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusimamishwa kwa mapigano hayo.