Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi afungwa jela kwa kumtusi Magufuli Tanzania

Bw Joseph Mbilinyi Haki miliki ya picha HISANI
Image caption Bw Joseph Mbilinyi (wa kwanza kushoto)

Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema Joseph Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kufungwa jela miezi mitano.

Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba mwaka mwaka jana jijini Mbeya.

Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini Mbeya.

Hati ya mashtaka imesema maneno waliyoyatamka yalienda kinyume na Sehemu 89(1) a ya Sheria za Jinai ambayo inaharamisha kutumiwa kwa lugha ya matusi.

Maneno hayo, hati za mashtaka zinasema, yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii