Wakuu wa majeshi wafutwa Saudi Arabia

Saudi Arabia's King Salman bin Abdulaziz (C)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

King Salman (katikati) aliingia madarakani mwaka 2015

Saudi Arabia imewafuata makamanda wa vyeo vya juu jeshini akiwemo mkuu wa majeshi.

Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Taarifa hizo zilichapishwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA, lakini hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa makamanda hao.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati vita nchini Yemen, ambapo muungano unao ongozwa na Saudi Arabia unaopigana na waasi unaelekea kumaliza mwaka wake wa tatu.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Muungano unaoongozwa na Saudia Arabia uliingia Yemen Machi 2015

Mrithi wa ufalame Mohammed bin Salman, ambaye pia ni waziri wa ulinzi anaaminiwa kuhusika kwenye mabadiliko hayo.

Mwaka uliopita watu mashuhuri nchini Saudi Arabia wakiwemo wanawafalme, mawaziri na wafanyabiashara matajiri walifungiwa kwenye hoteli ya kifahari ya Ritz-Carlto, wakatai mwanamfalme huyo aliongoza mikakati dhid ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.