Watu 7 wafariki Nigeria baada ya msichana Mkristo kuslimu na kuwa Mwislamu

Watu saba wafariki Nigeria baada ya baada ya msichana Mkristo kuwa Muislamu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu saba wafariki Nigeria baada ya baada ya msichana Mkristo kuwa Muislamu

Takriban watu saba wameuawa katika vita ambavyo vilizuka baada ya msichana wa dini ya Kikristo kubadili dini na kuwa Mwislamu Kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Vita hivyo vilivyozuka katika jimbo la Kaduna viliwaacha watu 15 wakiwa na majeraha baada ya nyumba kuchomwa moto.

Shahidi mmoja aliambia BBC kwamba tatizo lilianza baada ya msichana huyo wa Kikristo kutoka Gwari kubadili dini na kuwa Muislamu kutokana na ushawishi wa mpenzi wake.

Shahidi anasema kuwa tatizo hilo liliwachochea vijana wa Kikristo .

Ripoti nyengine zinasema kuwa wasiwasi kati ya wafuasi wa dini hizo mbili ulikuwa tangu awali.

Huwezi kusikiliza tena
Uzito wa dini katika kampeni za uchaguzi Marekani

Hata hivyo kamanda wa polisi wa Kaduna Muktar Aliyu aliambia BBC kwamba huku wakifanikiwa kuwakamata watu 10 wanaohusianana na kisa hicho, maafisa bado wanachunguza sababu ya vita hivyo.

''Hatuwezi kuthibitisha kwamba vita vilizuka kwa sababu kuna mtu alibadilisha dini na kuwa Mwislamu ama dini nyengine yoyote ile'', alisema.

''Watu wana haki ya kubadili dini na kuingia dini nyingine yoyote ile, hatua hiyo haifai kuchochea vita''.

Image caption Kanisa

Anasema kuwa hatua zimechukuliwa kuzuia vita hivyo kuenea kutoka Kasuwan Magani eneo ambalo ni kilomita 36 kutoka mji mkuu, hadi maeneo mengine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii