Trump amtaja Parscale kama meneja wa kampeni zake za 2020

Trump anaamini Parscale atasaidia kushinda tena kiti cha urais
Image caption Trump anaamini Parscale atasaidia kushinda tena kiti cha urais

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020.

Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni za Trump 2016 na alisifiwa sana kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri jambo linalotajwa kumpa ushindi Trump.

Parscale atatumika katika kampeni za uchaguzi mdogo baadae mwaka huu.

Image caption Brad Parscale anatajwa kuwa amebobea vilivyo katika masuala ya mitandao

Trump anasema Parscale ni mtu sahihi na amekuwa akifanya kila kitu kwa uhakika wa hali ya juu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii