Korea Kaskazini 'inaisaidia Syria na silaha za kemikali'

A Syrian man wears an oxygen mask at a make-shift hospital following a reported gas attack on the rebel-held besieged town of Douma in the eastern Ghouta region on the outskirts of the capital Damascus on January 22, 2018.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kumekuwa na ripoti hivi karibuni ya mashambulio kutumia gesi ya Chlorine eneo la mashariki ya Ghouta

Korea Kaskazini imekuwa ikiwatumia vifaa Syria ambavyo vinaweza tumika katika kutengeneza silaha za kemikali, ripoti ya chombo cha habari Marekani imesema kikinukuu ripoti kutoka Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo haijatolewa, wataalam wa bakora Pyongyang wameonekana katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria, gazeti la New York Times imesema.

Shutuma hizo zinakuja baada ya ripoti mpya ya utumiaji wa gesi ya chlorine na vikosi vya Syria, shutuma hizo zimekanushwa na serikali.

Korea Kaskazini ipo chini ya vikwazo vya kimataifa sababu ya programu yao ya nuklia.

Vifaa hivyo vinaripotiwa kupatikana kiwizi na kutumwa Syria na Korea Kaskazini vikiwemo vigae venye uwezo wa kuzuia joto na tindi kali mwingi na vipima joto. Vigae vinasemekana kutumika katika kujenga majengo ambapo silaha za kemikali zitatengenezwa.

Inasemekana wamtumiwa makumi ya mizigo ndani ya miaka kadha.

Gazeti hilo linasema, taasisi ya utafiti ya maswala ya sayansi ya Syria inasemekana kuwalipa Korea Kaskazini kupitia makumpuni bandia.

Serikali ya Syria imeripotiwa kuiambia Umoja wa Mataifa kuwa raia wa Korea Kaskazini waliopo Syria ni makocha na wanariadha tu.

Syira iliungana na mkutano wa silaha za kemikali na kukubali kuteketeza silaha hizo mwaka 2013 baada ya shambulio lililotumia gesi ya sarin na kuwaua mamia ya watu Ghouta.

Tangu mwaka huo, imeshutumiwa kwa kutumia silaha hizo marufuku mara kwa mara katika vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe.