Mwimbaji Misri afungwa kwa kuikashifu mto Nile

Sherine ni mwanamuziki maarufu nchini Misri Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sherine ni mwanamuziki maarufu nchini Misri

Mwimbaji wa Misri Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita gerezani kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile.

Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- alimwambia mashabiki wake kuwa kunywa maji kutoka mto huo kunaweza kumpatia vijidudu.

"Kunywa Evian badala yake." akatania

Mwimbaji mwingine, Laila Amer, pia alihukumiwa siku ya Jummane kifungo cha miaka miwili kutokana na video ya muziki.

Bi Amer - ambaye hana umaarufu kama Sherine - alipatwa na hatia ya 'kuchochea ufitini na uovu". Muongozaji wa kipindi na muigizaji walihukumiwa kwa vipindi vifupi.

Sherine, amehukumiwa na mahakama moja Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.

Mzaha

Mashtaka dhidi ya Sherine yalifunguliwa mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya mto Nile?).akajibu ''Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho''. Kichocho ni ugonjwa unaojitokeza maeneo ya vijijini nchini Misri.

Mbali na kesi dhidi yake, Chama cha wanamuziki nchini humo kimetangaza kuwa kimempiga maruguku kuuimba wimbo huo kuhusu Misri.

Abdel Wahab baadae aliomba radhi kutokana na tukio hilo akiwa kwenye tamasha lililofanyika huko Jumuia ya falme za kiarabu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Another singer, Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu

Haki miliki ya picha Shyma
Image caption Mwanamuziki Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu

Maamuzi ya mahakama yaliyotolewa siku ya Jumanne inafanya idadi ya wanamuziki kuhukumiwa kifungo kufikia watatu miezi ya hivi karibuni

Mwezi Desemba, Shaimaa Ahmed ajulikanaye kifupi Shyma alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kuonekana kwenye Video ya muziki akiwa amevalia nguo za ndani huku akila ndizi kwa mbwembwe.

alikutwa na hatia ya kuweka video yenye maadili mabaya akahukumiwa sambamba na muongozaji wa video hiyo.Baadae hukumu ilipunguzwa na kuwa ya mwaka mmoja baada ya kukata rufaa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii