Kim amuonyesha mtoto wake mtandaoni

Kim Kardasian Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Kardasian

Mwanamama Nyota nchini Marekani,Kim Kadarsian ameweka picha yake na mtoto wake Chicago mtandaoni

Chicago ni mtoto wake wa tatu kuzaa na Kanye West, alizaliwa na mwanamke aliyebeba mimba kwa niaba ya Kim tarehe 15 mwezi Januari.

Picha ya Kim ilipendwa mara milioni sita katika kipindi cha saa tisa.

Kim mwenye umri wa miaka 37 ameongelea kuhusu uamuzi wao wa kupata mtoto kwa njia ya kupandikiza kwa mwanamke mwingine, akisema kuwa yeye na mumewe tayari walikuwa na ukaribu na Chicago.

''Kanye na mimi tunafurahi kutangaza kuja kwa mtoto wetu mzuri wa kike'',Kim aliandika kwenye mtandao wake mwezi Januari.

''tunashukuru kwa mwanamke aliyefanikisha ndoto zetu na madaktari na wauguzi kwa uangalizi wao.

''North na Saint wamefurahi sana kumkaribisha dada yao''.

Kim alibeba mimba ya watoto wake wawili North wa miaka minne na Saint mwenye miaka miwili.

Lakini madaktari walimshauri Kim asibebe mimba tena kwa sababu ya uwezekano wa kupata shida kwenye uzazi.

Kim ana tatizo kitaalamu kinaitwa placenta accreta, ambapo kondo la nyuma hubaki likiwa limejishikilia kwenye kuta za mji wa mimba.