Mmarekani mpenzi wa jinsia moja aliyeikimbia Afrika

Mahad Olad

Chanzo cha picha, Ex-Muslims of North America

Maelezo ya picha,

Mahad Olad

Teksi ya usiku kwenda ubalozi wa Marekani; safari ya dharura kurudi nyumbani; maisha mapya mjini New York. mwislamu wa zamani anaelezea hadithi yake.

Mahad Olad alikuwa kwenye chumba cha hoteli mjini Nairobi akimtazama mama yake. Alikuwa akishika makala mbili kutoka kwa gazeti la wanafunzi la mjini New York.

Katika makala ya kwanza Mahad ambaye wakati huo alikuwa na miaka 19, alikuwa amesema alikuwa aamini kuwa Mungu yupo.

Kwenye makala ya pili alisema alikuwa mpenzi wa jinsia moja.

Mama yake ambaye ni muislamu wa asili wa Somalia hangeweza kamwe kukubaliana na hilo. Alisema angemtuma kwa kundi la mashehe.

Wasomali hao mashehe wangembadili, wamrejeshe katika jamii, kumfanya kuwa Muislamu na kumwachisha kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Mahad alikuwa amesoma kuhusu suala la wapenzi wa jinsia moja Afrika, mafunzo marefu ya kidini na mateso na hivyo hakutaka kushiriki.

Alikuwa amefurahia kuwa mpenzi wa jinzia moja na pia alikuwa na furaha kuwa mislamu wa zamani.

Alitikisa kichwa, akatabasamu na kumuambia mama yake angefanya vile alisema. Kisha baada ya kuondoka chumba cha hoteli, Mahad alipiga simu.

Mara baada ya mlango mmoja kufunga mwingine ukafunguka.

Waislamu wa zamani nchini Marekani ni kundi la watu wanaosi uislamu. Kauli mbiu yao ni: tunatamani ulimwengu ambapo kila mtu yuko huru kufanya kile moyo wake unamuambia.

Wengi wa wanachama wao ambao mara nyingi ni watoto wa wahamiaji hutengwa na familia zao, wengine hupokea vitisho vya kuuawa. Mahad alikuwa anahitaji msaada wao.

Kutoka chumba cha hoteli alimpigia simu mwanachama wa kikundi cha waislamu wa zamani huko Minneapolis, ambo ni mji alikulia. Kundi hilo liliwasiliana na ubalozi wa Marekani mjini Nairobi.

Wamarekani walikuwa na furaha kusaidia - Mahad ni raia wa Marekani - lakini kulikuwa na tatizo.

Ubalozi ulikuwa kwenye barabara ya shirika la Umoja wa Mataifa, mtaa wa majengo makubwa na vidimbwi vya kuogelea.

Mahad alikuwa hoteli umbali wa zaidi ya kilomita 10 mtaani Eastleigh, wanakoishi wasomalia wengi ambao pia unafahamika kama Mogadishu ndogo.

Wafanyakazi wa ubalozi hawaendi mtaa huo.

Kikudi hocho kilizungumza na wanachama wao wasomalia, amba waliwasiliana na wengine huko Eastleigh. Teksi ya usiku ilipangwa. Sasa Mahad alistahili kuondoka bila kujulikana.

Mahad alikuwa nchini Kenya na mama yake, ndugu yake mkubwa, dada mkubwa, dada mdogo na wapwa wawili. Pasipoti yake ilikuwa chumba cha mama yake, aliiingia kimya kimya na kuichukua wakati mama yake alikuwa bado amelala na kuteremka ngazi.

Mahad aliangalia tena kuhakisha kuwa ndugu yake hakuamuona. Alikuwa bado hajalala na kama angegundua angemzuia kuondoka.

Kwa hofu, Mahad alitoka nje. Akapata teksi akaingia ndani na kuondoka.

Kwenye ubalozi, aliwaonyesha walinzi paspoti ambao walimruhusu kuingia.

Afisa wa Marekani alikuwa anasubiri. Alimhoji Mahad na kumruhusu kukaa kwenye nyumba yake.

Siku nne baadaye baada ya kuwasili kwenye ubalozi. Mahad aliondoka Kenya kwa kutumia teketi aliyolipigwa na kundi la waislamu wa zamani, baada ya safari tatu aliwasili Ithaca, New York ambapo anasoma .

Haya yalitokea Mei 31 mwaka 2017. Hajaonekana au kuzumguza na familia tangu wakati huo.

Alizaliwa nchini Kenya mwaka 1997, baada wa wazazi wake wasomalia kukimbia vita. Mwaka 2001 familia yake ilihamia Minneapolis, Minnesota.

Wakati akiwa na umri wa miaka 13 au 14 walirudi nchini Kenya kwa karibu mwaka mmoja. Mahad alifurahia . Alihudhuria Madrassa- mafunzo ya dini ya kiislamu na hakutilia shaka dini yake.

Chanzo cha picha, Mahad Olad

Maelezo ya picha,

Nilishangaa na kujiuliza, hili ndilo dini yangu inaunga mkono. Hili ndilo uislamu unasimama nalo

Na kisha Septemba mwaka 2012 guruneti ikatupwa.

"Ilifanyika hatua chake kutoka kwangu," anasema. Walishambulia kanisa. Nilikimbia kuokoa maisha yangu."

Wanamgambo wa kislamu walirusha kilipuzi kwenda kwa kanisa moja la watoto. Mtoto mmoja aliuawa, watatu wakajeruhiwa vibaya. Usiku huo Mahad alisikia mwalimu wa dini ya kiislamu akihubiri.

"Alisema shambulizi hilo lilistahili kufanyika."

"Nilishangaa na kujiuliza, hili ndilo dini yangu inaunga mkono. Hili ndilo uislamu unasimama nalo. Kama ni kweli dini ya kislamu ina uhusiano na ghasia, basi sifikiri ninaweza kujitambua kuwa Muslim."

Wakati familia ilirudi Minnesota, Mahad alisema alisoma sana mitandaoni au kuchukua vitabu kutoka maktaba akifificha kutoka kwa familia yake.

"Ningesoma vitabu vya watu kama Richard Dawkins na Christopher Hitchens. Hivyo ndivyo nilianza kufahamu kuhusu jinsi nilihisi.

Kwa kugundua kikundi cha waliokuwa waislamu wa Marekani ambao wakati huo walipatikana kwenye mtandao wa Reddit tu kilichangia.

"Wakati huo ndio niligundua kuwa kulikuwa na jamii ya watu ambao wana matatizo haya pia na wanajiita waliokuwa waislamu," anasema. "Hata singefikiria kuhusu jina hilo, hata sikujua lilikuwepo."

Wakati huo ndio Mahad aligundua kuwa alikuwa mpenzi wa jinsia moja.

Baba yake Mahad alikuwa mwalimu wa dini katika Madrassa, mama yake alifanya kazi kwa shirika moja la kijamii. Mahad alikuwa kijana ambaye alijipata kati kati ya tamaduni mbili.

"Kwa kujitangaza kuwa mpenzi wa jinsia moja na kutoamini kuwepo kwa Mungu ni kinyume na tamaduni yangu na dini yangu," anasema. Si kitu ambacho wazazi wangu na familia wanaweza kamwe kukubali.