Siku ya 100: Mwandishi Azory Gwanda yuko wapi?

Siku ya 100: Mwandishi Azory Gwanda yuko wapi?

Zimetimia siku 100 tangu kutoweka kwa Mwandishi Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania aliyetoweka mwezi wa Novemba mwaka jana.

Francis Nanai Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, MCL, amesema wataisaida familia ya mwandishi huyo kwa kulipia ada za watoto,bima ya afya na mtaji biashara kwa mke wa Azory ili aweze kujikwamua kiuchumi.