Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria

Kusitishwa kwa mapigano kungesaidia ugawaji wa misaada ya kibinaadam
Image caption Kusitishwa kwa mapigano kungesaidia ugawaji wa misaada ya kibinaadam

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeambiwa kuwa vifo, uharibifu mkubwa na taabu vimeendelea kutokea eneo la Ghouta nchini Syria, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mkuu wa masuala ya dharura wa umoja wa mataifa Mark Lowcock, amesema vita vinavyoendelea na kuzuiliwa kuingia katika eneo walilopo raia wa kawaida inamaanisha kuwa hakuna msaada utakaoweza kuwafikia.

Image caption Mali na maisha ya watu yamekuwa hatarini kwa sababu ya vita

Ameongeza kuwa kusitishwa mapigano kwa saa tano pekee hakutoshi kuwafikia maelfu ya watu waliomo sehemu hiyo.

Wajumbe wa Marekani wameilaumu serikali ya Syria na washirika wake kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.

Mjumbe wa Urusi amesema waasi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake ndio wakulaumiwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii