Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 04.03.2018

Ryan Sessegnon. Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Ryan Sessegnon.

Manchester City watamenyana na mahasimu Manchester United na Tottenham kumsainia beki wa Fulham kijana wa miaka 17 Ryan Sessegnon. (Sunday

Meneja wa West Brom Alan Pardew yuko kwenye hatari ya kupoteza kazi yake baada ya kipigo cha Jumamosi kutoka Watford. (Sunday Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Craig Dawson

West Brom wanajiandaa na kuondoka kwa wachezaji wengi ikiwa watashuka katika jedwali ambapo mlinzi wa Northern Ireland Jonny Evans, 30, kipa wa England Ben Foster, 34, mlinzi wa England Craig Dawson, 27, na msambulizi wa England Jay Rodriguez, 28, ambao wote wanavutia vilabu vingine. (Sun on Sunday)

Meneja mjerumani Joachim Low anaibuka kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Carlo Ancelotti

Arsenal na Chelsea watang'ang'ana kupata huduma zake Carlo Ancelotti kama meneja mwisho wa msimu. (Sunday Express)

Arsenal wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27, wakati klabu hiyo inataka kuzuia kumpoteza bila kunufaika msimu wa joto mwaka 2019.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David de Gea

Manchester United watampa kipa David de Gea, 27, mkataba mpya wa paunia 350,000 kwa wiki kumzuia kujiunga na Real Madrid. (Daily Star on Sunday)

Everton wanampango wa kumsaini mshambulizi wa England Jamie Vardy kutoka Leicester na mchezaji huyo wa miaka 31 ni namba moja kati ya wachezaji klabu hiyo inataka kuwasaini.(Sunday Mirror)

Image caption Jeam Michael Seri

Liverpool wanaongoza mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Nice Jeam Michael Seri huku Arsenal, Manchester United na Tottenham wakimmezea mate mchezaji huyo wa miaka 26.

Meneja wa Celtic Brendan Rodgers amahusishwa na kuchukua mahala pake Arsene Wenger huko Arsenal, lakini Rodgerd anasema anaishi kwa ndoto yake katika klabu hiyo ya Scottland. (ESPN)

Wing'a wa Brazil Willian, 29, anasema anataka kusalia Chelsea kwa muda mrefu lakin amekiri kuwa ataondoka ikiwa hawamhitaji. (Planeta SporTV via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic anasema kuwa kusaini kenye ligi kubwa nchini Marekani iko akilini mwake. Mchezaji huyo wa miaka 36, anatarajia kundoka Manchester United mwisho wa msimu. (Sky Sports)

Liverpool wameanza mazungumzo ya mkataba na mshambualiaji wa Brazil Robert Firmino. Meneja Jurgen Klopp anesema mchezaji huyo wa miaka 26 anastahili kupewa mkataba mpya. (Metro)

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola anasena hakuna tofauti kati ka Pogba 24, na meneja wa Manchester United Jose Mourinho. (Rai Sport via Mail)

Mada zinazohusiana