Nyota wanamuombea Rick Ross aliyelazwa hospitalini

Rick Ross

Missy Elliot na Snoop Dogg ni miongoni mwa nyota wanaomuombea rappa Rick Ross aliyelazwa hospitalini Marekani.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 42 amelazwa katika hospitali moja huko Miami, huku taarifa zisizoweza kuthibitishwa kutoka vyombo vya habari nchini humo zikiashiria kwamba yuko katika hali mahututi.

Katika matandao wa kijamii Twitter Snoop aliandika "Maombi kwa wingi kwa rafiki yangu Rick Ross", "Tunatumai utapona ndugu yangu."

Haijulikani wazi anaugua nini kwa sasa.

Missy Elliot amesema yeye pia anamuombea muimbaji huyo wa mtindo wa rap ambaye pia ni mfanyabiashara.

Nyimbo za Diamond na wengine zafungiwa Tanzania

Miongoni mwa marafiki wake Ross mashuhuri P Diddy alituma ujumbe katika mtandao wake wakijamii akitaka kila mtu amuombee Rick Ross.

Fat Joe na LL Cool J wameelezea wasiwasi wao, huko LL Cool J akimuambia Rick "Vumilia".

Familia ya Rick Ross imekana taarifa kwamba mwanamuziki huyo amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Na rappa Fat Trel, aliyesajiliwa na kampuni ya muziki ya Ross amesema "hajambo" na hakuekwa katika mashine hiyo ya kusmaidia kupumua.

Rick Ross, ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts II, alifafatika mara mbili katika muda wa saa 6 mnamo 2011.

Wakati huo alisema alifafatika kutokana na ukosefu kupumzika.

"Nitalala saa mbili alafu nishughulike - Kwasababu ya kutafuta riziki - u hustler," alisema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii