Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 05.03.2018

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Everton wanataka Arsene Wenger kuwa meneja wao ikiwa atafutwa na Arsenal. Mmliki wa klabu ya Everton Farhad Moshiri anaamini kuwa Wenger ni bora zaidi kuisaidia Everton kujijenga. (Star)

Chelsea wana mpango wa kumleta mchezaji wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta katika safu yake ya usimamizi. (Mirror)

Arsenal wanataka mrithi wa Wenger kuwa kocha mkuu badala ya meneja, hatua ambayo itampa fursa zaidi ya kufunza.(Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thierry Henry

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, anasema atakubanli ikiwa ataombwa kuchukua mahala pake Arsen Wenger. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, anasema lawama dhidi yake kwa kuhamia Anfield kutoka Arsenal ni upuzi akisema kuwa lawama hizo hazima athari yoyote kwake.(Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Oxlade-Chamberlain

Mashambulizi wa Brazil Willian, 29, anasema anataka kusalia katika klabu hiyo ya Premier League licha Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini (Planeta Sportv - in Portuguese)

Tottenham wanamtaka mchezaji wa Bayer Leverkusen mlinzi raia wa Ujerumani Jonathan Tah, 22 kuchukua mahala pake Toby Alderweireld. Tottenham wameshindwa kuafikiana mkataba mpya na mchezaji huyo wa miaka 29. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Paris Saint-Germain hawatamuuza Neymar mwisho wa msimu, kwa mujibu wa mkurugenzi Antero Henrique, licha ya mchezaji huyo wa miaka 26 kuhusishwa na Real Madrid. (Goal via L'Equipe)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema haelewi vizuri kuhusu kikosi watakutana nacho Jumatatu usiku cha Manchester United. (Sun)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Ryan Sessegnon

Manchester City watamenyana na mahasimu Manchester United na Tottenham kumsainia beki wa Fulham kijana wa miaka 17 Ryan Sessegnon. (Sunday

Meneja wa West Brom Alan Pardew yuko kwenye hatari ya kupoteza kazi yake baada ya kipigo cha Jumamosi kutoka Watford. (Sunday Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Craig Dawson

West Brom wanajiandaa na kuondoka kwa wachezaji wengi ikiwa watashuka katika jedwali ambapo mlinzi wa Northern Ireland Jonny Evans, 30, kipa wa England Ben Foster, 34, mlinzi wa England Craig Dawson, 27, na msambulizi wa England Jay Rodriguez, 28, ambao wote wanavutia vilabu vingine. (Sun on Sunday)

Meneja mjerumani Joachim Low anaibuka kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana