Nembo za bidhaa za Afrika zinaweza kufanikiwa kimataifa?

Bidhaa za urembo zitang'ara kwenye masoko ya kimataifa? Haki miliki ya picha LUXURY CONNECT AFRICA
Image caption Bidhaa za urembo zitang'ara kwenye masoko ya kimataifa?

Nembo za bidhaa za urembo na mapambo kutoka kwenye bara la Afrika zinaongezeka kwa kasi na kuna matumaini kuwa huenda yakaja kuwa majina maarufu mno kwa kizazi kijacho.

Soko la bidhaa za mapambo duniani lina thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.5, kwa mujibu wa utafiti wa Bain &Company inayojihusisha na ushauri wa masuala ya biashara kimataifa.

Soko hili linatarajiwa kukua kwa 5% kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wimbi la bidhaa hizi linalowalenga watumiaji wakubwa linaweza kumaanisha kuwa bidhaa kutoka Afrika zinaweza kuanza kushindana na zile zenye majina maarufu duniani.

Imeelezwa, kuwa soko la bidhaa za mapambo bado linafanya vizuri katika nchi za Ulaya na Marekani.

Nchini Tanzania, tayari mwanamuziki Diamond Platnumz ameanza juhudi za kutumia nembo yake kuuza bidhaa, ambapo ana manukato na hata njugu karanga.

Swali ni kuwa lini tutaona majina ya bidhaa za Afrika zikishika nafasi sambamba na majina makubwa yanayoongoza duniani?

Haki miliki ya picha LUXURY CONNECT AFRICA
Image caption Vania Leles anasema amehamasishwa sana na Afrika katika kazi zake

Vania Leles ni mmoja kati ya waafrika wengi wanaomiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa kwa majina yao barani Afrika.

Alizaliwa na kukulia Guinea-Bissau,mtaalamu huyu wa masuala ya vito alifungua duka lake la bidhaa za vito jijini London liitwalo Vanleles Diamonds mwaka 2011.

Miaka saba sasa, duka lake liko Mayfair, liko kati ya bidhaa maarufu za Ufaransa Cartier na Chanel.

Anasema kuwa Afrika ni chanzo cha yeye kufika hapo, hasa kumbukumbu za alipokuwa mtoto, kumbukumbu za kusafiri barani afrika.

Alisafiri katika nchi 15 alipokuwa na miaka kati ya 15 na 18.

Vito vingi vilivyotumika kwenye duka lake la sonara vyanzo vyake ni Afrika, alisema

''Pengine ni asilimia 80 mpaka 90 ya (mawe na almasi) vinatoka Afrika, lakini huoni bidhaa zikiwa na utambulisho huo: kwa mfano 'Almasi hii ni kutoka Botswana'. Nafikiri imefika muda sasa kuviinua vyetu,mali asili zetu".

Haki miliki ya picha LUXURY CONNECT AFRICA

Bi Leles anaeleza umaarufu wa mawe ya zumaridi (emerald) kutoka Colombia na rubi kutoka Burma ni maarufu kwa sababu ya chapa yake na katika kutangaza.

''Kumekuwa na uwekezaji mkubwa kwenye soko ''.

''Lakini kwa uzuri na uthamani zumaridi ya Zambia ni bora zaidi ni nzuri sana, ni kumwelekeza tu mtumiaji kwa ujumla kuhusu kipi bora zaidi''.

Lele hufanya bidhaa zake zitambulike wapi zilikotoka tofauti na masonara wengine.

Bidhaa za uzuri wa ngozi nyeusi Hongkong

Duka la Harrods linauza bidhaa ya ngozi Espara Skin Care, bidhaa ya urembo uliochanganywa na vikorombwezo kama vile mafuta ya argan, shear butter na Liquorice. Kila kikopo kina gharama yake ya zaidi ya dola 100.

Haki miliki ya picha EPARA SKINCARE

Mwanzilishi wa Epara, Ozohu Adoh alibuni chapa hii maalum kwa ajili ya kueleza uzuri wa rangi ya mwanamke, lakini akagundua kuwa bidhaa hii ilipanuka hata hata ikafika nje ya soko alilolikusudia.

''Nilidhani soko letu kubwa litakuwa London na maeneo ya nchi chache Afrika.Nikashangazwa sana nilipozungumza na wakala mmoja Hong Kong akisema wangependa kuuza bidhaa huko.imekuwa na mahitaji makubwa zaidi mpaka leo''.

Bi Adoh anasema bidhaa yake imependwa na wanawake wa kila aina.

Haki miliki ya picha LUXURY CONNECT AFRICA
Image caption Uche Pezard (kushoto)

Kampuni zaidi na zaidi kama Vanleles na Epara zinaingia kwenye soko la dunia na yanafanya vizuri, bidhaa kama za Chanel na Hermes zimejengwa kwa karne zimekuwa na muda mwingi wa kujiendeleza na kutambulika dunia nzima.

Watu kama wanaotoa ushauri kuhusu chapa za bidhaa Uche Pezard anafikiri teknolojia inaweza kusaidia kubadili mwelekeo kwa wale wanaoibukia kwenye soko la bidhaa za mapambo kuacha alama zao wakakumbukwa.

Bi Pezard mwanzilishi wa Luxury Connect Africa, anasema amebaini uwepo wa mahitaji makubwa ya bidhaa za mapambo kutoka Afrika. Bidhaa hizi zinatoka kwa watumiaji duniani kote si tu kwa waafrika walio Afrika na walio nje ya Afrika pekee.

Anasema ''Sasa hivi tuko kwenye miaka ambayo inafanya watumiaji wanafahamu kilichomo kwenye bidhaa kabla ya kutumia. Watu hutumia mitandao ya kijamii,na digitali kwa ajili ya kupata taarifa.

''Wateja kwa ujumla wanafahamu chapa za bidhaa, historia, chimbuko lake na watu wanavutiwa na hivyo kwanza kabla ya kununua bidhaa''.

Haki miliki ya picha LUXURY CONNECT AFRICA

Ukiongelea kuhusu jukwaa la biashara yake, Luxury Connect Africa, anaeleza malengo ya kusaidia kampuni za Kiafrika kufanya mabadiliko na kuwa biashara kubwa kimataifa.

Anawakilisha lebo za mitindo ya nguo kutoka Afrika Kusini, Maxhosa ya Laduma, mavazi ya Tiffany Amber wa Nigeria na mipango ya kuboresha wimbi la bidhaa za mapambo kutoka Afrika.

"Bidhaa za kutoka Afrika hazijatayarishwa kiasi cha kuweza kushindana sokoni, zinakosa mipango kabambe ya kibiashata, hata hivyo hali hii inabadilika.

''Wabunifu, watengenezaji na wagunduzi na wajasiriamali wameanza kutumia fursa hizo za kufikia soko kimataifa iwe kwa kutumia biashara mtandaoni au kusafiri kimataifa. Wanaanza kupata mwamko wa kuacha alama katika soko la kimataifa."

Mada zinazohusiana