Tillerson anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza barani Afrika

Marekani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson anatarajiwa kuanza ziara katika mataifa matano ya Afrika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani humo.

Katika juma moja ya ziara yake atazitembelea Chad, Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Kenya.

Safari hii iliyoelezwa kuwa ya muhimu kwa Marekani kuchukua nafasi ya kuwa sehemu ya ukuaji wa maendeleo ya Afrika.

Tillerson anatarajiwa kuwasili nchini Ethiopia kesho Jumatano, nchi ya pili yenye idadi ya kubwa zaidi ya watu barani Afrika na moja ya taifa lenye kukua uchumi kwa kasi barani Afrika.

Hata hivyo Ethiopia bado inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa bada ya kujiuzulu kwa ghafla kwa waziri mkuu wanchi hiyo na zaidi ya miaka mitatu ya maandamano ya kuipinga serikali.

Maafisa wa Marekani wanasema Tillerson atakutana na viongozi Ethiopia kujadili mchakato wa atakayechukua uongozi na kuhusu vurugu zilizojitokeza na vilevile kiongozi huyo ataongea na viongozi wa umoja wa Afrika ili kuzungumzia juu ya migogoro iliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Somalia na Sudan Kusini.

Baadae wiki hii ataelekea Kenya, Nigeria, Chad na Djibouti ambayo Marekani inaona ni washirika wake wa karibu wa kupambana na Ugaidi na kuleta usalama katika upande wa kikanda.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii