Ilikuwaje leo Machi 8 ikawa Siku ya Wanawake Duniani?

Siku ya kimataifa ya Wanawake mjini Diyarbakir, Uturuki mwaka 2016 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku ya kimataifa ya Wanawake mjini Diyarbakir, Uturuki mwaka 2016

Huenda umeshuhudia siku ya Wanawake Duniani ikitajwa kwenye Vyombo vya Habari au kusikia kwa marafiki .

Lakini kwa nini? Lini? Je ni sherehe au maandamano? na Je kuna siku kama hiyo ya kimataifa kwa Wanaume?

Kwa zaidi ya karne sasa, watu duniani wamekuwa wakisherehekea siku hii.

1. Ilianzaje?

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.Kilikuwa chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadae.

Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina Clara Zetkin.

Alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Kulikuwa na wanawake 100 hapo kutoka nchi 17 na wakakubaliana kwa pamoja.

Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.

Sherehe ya 100 ilifanyika mwaka 2011, hivyo mwaka huu ni sherehe ya 107 ya wanawake duniani.

Haki miliki ya picha Topical Press Agency
Image caption Clara Zetkin alianzisha siku hii mwaka 1910

Suala hilo likawa rasmi mwaka 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuanza kusherehekea siku hiyo na baadae kubuni kauli mbiu.Ya kwanza mwaka 1996 ilikuwa ''furahia yaliyopita, panga kwa ajili ya baadae''.

Siku ya kimataifa ya wanawake duniani imekuwa siku ya kutathimini maendeleo ya wanawake katika jamii katika nyanja za siasa na uchumi, kulikuwa pia na migomo na maandamano yaliyoratibiwa kwa ajili ya kusisitiza masuala ya usawa.

2.Ilikuwalini?

Tarehe 8 mwezi Machi. Wazo la Clara Zetkin la Siku ya kimataifa ya wanawake duniani halikuwa na tarehe maalum na haikuwa rasmi mpaka kipindi cha vita ya mwaka 1917 wakati wanawake wa kirusi walipodai Amani na kufanyia kazi tatizo la upungufu wa chakula (Waliimba Amani na Mkate).

Siku nne za mgomo, zilifanya watawala wa Urusi kuwapa wanawake haki ya kupiga kura.Tarehe ambayo mgomo ulianza ulikuwa kwenye kalenda ya Julian, ambayo ilikuwa ikitumika Urusi wakati huo, ilikuwa siku ya Jumapili tarehe 23 Mwezi Februari.

Siku hii katika kalenda ya Gregoria ilikuwa tarehe 8 mwezi Machi.

Na ndio hii inayosherehekewa leo.

3.Je kuna siku ya wanaume?

Ndio ipo, tarehe 19 Novemba. Lakini iliadhimishwa tangu miaka ya 90 na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa.Watu huiadhimisha katika nchi zaidi ya 60. Lengo la siku hii ni kutazama afya za wanaume na wavulana, kuimarisha mahusiano ya jinsia,usawa wa jinsia na kutathimini jinsia ya kiume kama watu wa mfano wa kuigwa.Kauli mbiu ya mwaka 2017 ilikuwa 'kuwaadhimisha wanaume na wavulana'

4.Siku ya wanawake duniani inaadhimishwaje duniani?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamke akiwa amebeba maua mjini Roma, siku ya Wanawake duniani mwaka 2012

Siku ya kimataifa ya wanawake ni siku ya mapumziko katika nchi nyingi ikiwemo Urusi, ambapo mauzo ya maua huwa mara mbili zaidi wakati wa siku tatu au nne kabla ya siku yenyewe, ambapo wanaume na wanawake huwapa maua wapendwa wao wa kike na wafanyakazi wenzao.

Nchini China, wanawake wengi hufanya kazi nusu siku tarehe 8 Machi, kama ilivyoshauriwa na Baraza la nchi hiyo ingawa waajiri si mara zote wanatekeleza utamaduni huo.

Nchini Italia, siku ya kimataifa ya wanawake au La Fiesta della Donna inasheherekewa kwa kupeana maua chanzo cha utamaduni huu hakifahamiki lakini inaaminika ilianzia Roma baada ya vita ya pili ya dunia.

Nchini Marekani, Mwezi Machi ni mwezi wa historia kwa wanawake. Rais hutambua kila mwaka na kuthamini mafanikio ya wanawake wa Marekani.

5. Mwaka huu kinafanyika nini?

Kampeni ya siku ya kimataifa ya wanawake ina kauli mbiu isemayo ''Chochea kwa ajili ya maendeleo''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Takriban watu 500,000 waliandamana Washington siku kama ya leo mwaka jana

Mwaka jana, mamilioni ya waandamanaji nchini Marekani na duniani kote wakipaza sauti kuhusu haki za wanawake baada ya ushindi wa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani.

Mwaka 2018 maelfu ya watu wameingia mitaani tena katika miji mbalimbali ya Marekani,kumpinga Rais na kuwahamasisha wanawake kujiandikisha kupiga kura.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii